Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ikiwa hakuna kitakachofanyika, njaa kote Gaza ni jambo lisiloepukika

Familia zinazokabiliana na njaa kali zikisubiri chakula huko Deir Al Balah, Gaza.
© UNRWA
Familia zinazokabiliana na njaa kali zikisubiri chakula huko Deir Al Balah, Gaza.

Ikiwa hakuna kitakachofanyika, njaa kote Gaza ni jambo lisiloepukika

Msaada wa Kibinadamu

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayouhusika na misaada ya kibinadamu yameonya leo Jumanne Februari 27 kupitia Baraza la Usalama lililokaa mahususi kwa ajili ya kujadili hali ya ukosefu wa chakulaPalestina kwamba ikiwa hatua hazitachukuliwa kurekebisha hali, njaa kote Gaza haitaepukika.

Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), Ramesh Rajasingham, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba hali ya Gaza ni mbaya, na karibu watu wote wanalazimika kutegemea "msaada wa chakula cha kibinadamu" ambao hautoshi kwa maisha.”

Amesema kuna hatari hali inaweza kuwa mbaya zaidi. "Operesheni za kijeshi, ukosefu wa usalama na vikwazo vingi vya kuingia na kuwasilisha bidhaa muhimu vimepunguza uzalishaji wa chakula na kilimo." 

Uharibifu mkubwa wa mfumo wa chakula

Maurizio Martina, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), pia limeeleza hali ya kutisha ya Gaza, wakati ambapo takriban wakazi 378,000 wanakabiliwa na umaskini. Awamu kali zaidi ya uhaba wa chakula.

"Matokeo makuu ya utafiti yanatia wasiwasi," ameonya, akitoa mfano wa madhara makubwa ya vita, kutoka kwa sekta ya uvuvi iliyopungua, ambayo ilitoa riziki kwa wakazi zaidi ya 100,000 wa Gaza, hadi vifo vingi vya mifugo kufuatia mashambulizi ya anga au ukosefu wa maji na lishe.

Viwango vya juu vya utapiamlo kwa watoto

Carl Skau, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), amesema Kamati ya Mapitio ya Njaa imeonya juu ya matarajio halisi ya njaa ifikapo Mei, huku watu 500,000 wakiwa katika hatari ikiwa tishio hilo litatokea. Leo, msaada wa chakula unahitajika na karibia watu wote, au watu milioni 2.2.

"Gaza ina kiwango kibaya zaidi cha utapiamlo wa watoto duniani," amesema na kuongeza kwamba mtoto mmoja kati ya sita walio chini ya umri wa miaka miwili anakabiliwa na utapiamlo mkali.

WFP iko tayari kupanua haraka na kuimarisha shughuli zake endapo kutakuwa na makubaliano ya kusitisha mapigano. Hatua za haraka zinahitajika ili kuwezesha ongezeko kubwa la kiasi cha chakula na vifaa vingine vya kibinadamu.