Watu milioni 10 DPRK wanakabiliwa na uhaba wa chakula:WFP/FAO

3 Mei 2019

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo kuhusu tathimini ya chakula kwenye Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea au DPRK imebaini hali ya kutia hofu ya watu kula chakula kidogo, kutokuwa na lishe inayostahilina familia nyingi kulazimika kupunguza idadi ya milo au kula kidogo sana.

Matokeo ya tathimini hiyo ya pamoja iliyofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO yanasema kufuatia mavumo mabaya katika kipindi cha miaka 10 yaliyosababishwa na ukame, ongezeko la joto na mafuriko takribani watu milioni 10.1 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula ikimaanisha kwamba hawana chakula cha kuwatosha hadi msimu mwingine wa mavuno.

Tathimini ya chakula

Makadirio ya uzalishaji wa chakula kwa mwaka 2018/2019 kwa mujibu wa ripota hiyo ni tani milioni 4.9 kiwango kidogo kabisa tangu msimu wa 2008/2009. Mbali ya changamoto hizo za tabianchi pia imeelezwa kuwa upungufu wa nyenzo za kilimo kama mafuta, mbolea na vipuri umechangia kwa kiasi kikubwa katika athari hizo.

Tathmini hiyo imetokana na ziara iliyofanywa na timu ya WFP na FAO nchini DPRK mwezi Novemba 2018 na mwezi Aprili mwaka huu ambayo imehitimisha kwamba kupungua kwa mavuno, kuongezeka kwa hasara baada ya mavuno, kumesababisha upungufu wa chakula wat ani milioni 1.36. 

Ripoti hiyo imeelezea hofu kubwa kuhusu ukosefu wa virutubisho vya mlo kamili ambao ni muhimu kwa lishe bora  na kusema “hali ni mbaya Zaidi kwa Watoto wadogo, kina mama wajawazito na wanawake wanaonyonyesha ambako wako katika hatari ya kupata utapiamlo.”

WFP/James Belgrave
Korea in April 2019. Wakulima wakijiandaa kupanda mpunga kaunti ya Sonchon Kusini mwa mkoa wa Hwanghae nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea au DPRK Aprili 2019.

Hali halisi

Pia ripota imebaini kwamba “Mfumo wa serikali wa ugawaji chakula ambao ndio unaotegemewa na asilimia kubwa ya watu nchini DPRK umelazimika kupunguza mgao wa chakula na kufikia kiwango kidogo sana kwa wati huu na kuna hofu kwamba kwa kutokuwepo msaada kutoka nje mgao huo huenda ukapunguzwa Zaidi katika miezi mibaya ya Juni hadi Oktoba ambayo nio miezi ya msimu wa muambo”.

Kwa mujibu wa Nicolas Bidault mshauri wa kikanda wa WFP na kiongozi mwenza wa tathimini hii “Familia nyingi kwa mwaka mzima zinaishi kwa kutegemea wali na Kimchi . 

Kimchi chakula maarufu nchini humo ambacho ni mchanganyiko wa matango na kabichi. Hii ni hali inayotia wasiwasi mkubwa kwa sababu jamii nyingi tayari ziko katika hali mbaya na kukata Zaidi mgao wa chakula kutawatumbukiza katika janga kubwa la njaa.”

Naye Mario Zappacosta afisa wa masuala ya uchuni wa FAO na kiongozi mweza wa tathimini hii amesema “Hofu yetu kubwa mwaka huu ni kuhusu mazao ya ngano, shayiri na viazi ambayo ni mazao yaliyo na jukumu muhimu y la kukidhi mahitaji ya chakula wakati wa msimu unaokuja wa muambo licha ya kwamba mazao hayo ni alimia 10 tu ya uzalishaji wa chakula DPRK. Tathimini yetu imeonyesha kwamba kupungua kwa mvua na theluji wakati wa msimu wa baridi hali ambayo iliyaacha mazao katika hali mbaya na kupunguza uzalishaji kwa asilimia 20.”

Nini kifanyike

WFP/James Belgrave
Wakulima wakijiandaa kupanda mahindi Kusini mwa mkoa wa Hwanghae nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea au DPRK Aprili 2019.

Miongoni mwa mapendekezo ya ripoti hiyo ni kuongeza msaada wa chakula ili kukidhi mahitaji ya dharura na kutoa kipaumbele kwa maeneo ambayo mahitaji ya chakula ni makubwa Zaidi na ambako athari za tabianchi ni kubwa.

Pia imependekeza kuongeza wigo wa  program za lishe na kupunguza athari za majanga ili kuziwezesha jamii kuwa na mnepo kwa majanga ya siku zijazo.

Mapendekezo mengine ni kuwa na mfululizo wa hatua za kupiga jeki uzalishaji wa kilimo ikiwemo kuingiza kutoka nje mbolea na madawa ya kilimo, pampu za maji, kilimo cha kisasa na mbegu za mbogamboga. Lakini pia kuboresha nyezo za kukausha chakula na maghala ya kukihifadhi ili kupunguza upotevu wa mavuno.

Kinachofanyika

WFP na FAO kazi yao hivi sasa DPRK ni kujikita na kutoa msaada wa lishe kwa watu 770,000 wenye utapiamlo wakiwemo wanawake na Watoto katika majimbo 9 nchi humo. Msaada huo ni pamoja na lishe ya nafaka na biskuti za kuongeza nguvu, mafuta na ptotini ambayo ni muhimu kwa afya bora na msaada huo unatolewa pia kwenye shule za chekechea, hospitali na kwenye vituo vya kulelea Watoto.

Pia FAo na WFP wanatoammsaada kwa Zaidi muungano wa wakulima 500,000 kwa kuwapa nyenzo muhimu za uzalishaji na pia kuanzisha mbinu na teknolojia itakayowasaidia katika kilimo endelevu kama cha mpunga na mchanganyiko wa kilimo na ufugaji, na pia kuwajengea mnepo wa kihimili mabadiliko ya tabianchi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud