Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi dhidi ya hospitali za Gaza ni ya kulaumiwa na lazima yakome: Griffiths

Hospitali ya Al Shifa inatumika kama makazi ya familia zilizohamishwa huko Gaza.
© WHO
Hospitali ya Al Shifa inatumika kama makazi ya familia zilizohamishwa huko Gaza.

Mashambulizi dhidi ya hospitali za Gaza ni ya kulaumiwa na lazima yakome: Griffiths

Amani na Usalama

Maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa leo Jumamosi waesema Jumamosi hakuwezi kuwa na uhalali wa vitendo vyovyote vya vita ndani au karibu na kituo chochote cha huduma ya afya, huku kukiwa na ripoti kwamba hospitali kubwa zaidi ya Gaza imeshambuliwa na vikosi vya Israeli wakati wanapambana na wanamgambo wa Kipalestina.

Katika taarifa, jeshi la Israel limekanusha kuwa lililenga hospitali ya Al-Shifa katika mji wa Gaza, ambayo wanadai iko juu ya kituo cha Hamas, lakini wamekiri kwamba mapigano yanatokea karibu na kituo hicho.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura , Martin Griffiths, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba kutokana na ripoti za kutisha za mashambuliz, kunaweza kuwa hakuna uhalali wa vitendo vya vita katika vituo vya afya vinavyowaacha watu bila umeme, chakula au maji na kuwashambulia kwa risasi wagonjwa na raia. wanaojaribu kukimbia.”

Amesisitiza kuwa “Hili ni jambo lisilofaa, ni la kulaumiwa na lazima likomeshwe. Hospitali zimekuwa sehemu za usalama zaidi na wale wanaozihitaji lazima waamini kuwa ni sehemu za makazi na sio za vita." 

Miundombinu ya raia isiingizwe vitani

Mratibu Mkaazi na Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika eneo linalokaliwa la Palestina, Lynn Hastings, ametilia mkazo wito wa kusitisha mapigano mara moja, akisisitiza kwamba miundombinu ya kiraia "haiwezi kutumika kwa operesheni za kijeshi. Wagonjwa, wahudumu wa afya na watu waliotawanywa wanaopata hifadhi lazima walindwe. Kanuni za uwiano, tofauti lazima ziheshimiwe."

Habari zilizonukuu shirika lisilo la kiserikali linalowakilisha madaktari, zilisema kuwa watoto wawili waliozaliwa kabla ya wakati wamekufa katika saa chache zilizopita huko Al-Shifa, baada ya jenereta ya mwisho kufanya kazi kuharibika wakati wa mashambulizi ya anga. Hospitali hiyo imeripotiwa kukosa maji, chakula na umeme.

Takwimu za hivi karibuni kutoka OCHA, zilizozipata kutoka kwenye wizara ya afya huko Gaza ambayo Umoja wa Mataifa unaiona kuwa ya kuaminika zinaripoti kwamba zaidi ya watu 10,800 wameuawa katika eneo hilo tangu mashambulizi ya Oktoba 7 na zaidi ya 26,900 kujeruhiwa.

Israel jana Ijumaa ilirekebisha idadi ya waliouawa kutokana na mashambulizi ya kigaidi ya Hamas ya Oktoba 7 kutoka 1,400 hadi 1,200.

Hospitali ya Al-Shifa huko Gaza. WHO yaonya kuwa hospitali katika Ukanda wa Gaza ziko katika hali mbaya.
WHO/Occupied Palestinian Territory
Hospitali ya Al-Shifa huko Gaza. WHO yaonya kuwa hospitali katika Ukanda wa Gaza ziko katika hali mbaya.

Maisha yako njiapanda

Mapema leo Jumamosi, shirika la Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto UNICEF limesema kwamba "kukaribia kusambaratishwakabisa na mashambulizi dhidi ya huduma za matibabu na afya, hasa kaskazini mwa Gaza, vimeacha maisha yakiwa katika hatari kubwa."

Shirikahilo limesema kuwa huduma za matibabu katika hospitali za watoto za Al-Rantisi na Al-Nasr katika Ukanda huo "zimeripotiwa kuwa karibu kukoma kwani ni jenereta ndogo tu iliyobaki kuwasha chumba cha wagonjwa mahututi. Haki ya watoto ya kuishi na afya inanyimwa," amesema Adele Khodr, Mkurugenzi wa UNICEF Mashariki ya Kati na Kanda ya Afrika Kaskazini. 

Ameongeza kuwa "Ulinzi wa hospitali na utoaji wa vifaa vya matibabu vya kuokoa maisha ni wajibu chini ya sheria za vita, na vyote viwili vinahitajika sasa."

Wakati huo huo, vituo vya matibabu katika maeneo ya kati na kusini mwa Ukanda wa Gaza, ambayo tayari vimezidiwa na idadi kubwa ya majeruhi wanaohitaji matibabu, sasa inabidi kukabiliana na kutibu mahitaji ya mamia ya maelfu ya watu kwenye msongamano mkubwa zaidi limebainisha shirika hilo la UNICEF.

"Huduma hizi zilizopo lazima ziungwe mkono na kuimarishwa ili kukabiliana na ongezeko la changamoto zinazowakabili. Maisha ya watoto yakohatarini" amesema Bwana Khodr akiongeza kuwa watoto wa kaskazini "hawana pa kwenda na wako katika hatari kubwa."