Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya watu wengi yanaendelea Ethiopia na kuhatarisha ukatili mkubwa zaidi: UN

Jamii zilizopo katika mazingira magumu wakipokea msaada wa chakula kutoka kwa Umoja wa Mataifa katika eneo la Tigray nchini Ethiopia.
© WFP/Michael Tewelde
Jamii zilizopo katika mazingira magumu wakipokea msaada wa chakula kutoka kwa Umoja wa Mataifa katika eneo la Tigray nchini Ethiopia.

Mauaji ya watu wengi yanaendelea Ethiopia na kuhatarisha ukatili mkubwa zaidi: UN

Amani na Usalama

Nchini Ethiopia, uhalifu wa kivita umeendelea bila kusitishwa karibu mwaka mmoja baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Serikali ya nchi hiyo na vikosi kutoka eneo la kaskazini la Tigray, amesema leo wataalam huru wa haki za binadamu walioteuliwa na Umoja wa Mataifa.

Ripoti ya hivi kribuni kutoka kwa tume ya kimataifa ya wataalamu wa Haki za binadamu kuhusu Ethiopia imeandika kuhusu ukatili unaofanywa na pande zote kwenye mzozo wa nchi hiyo tangu tarehe 3 Novemba 2020 ambayo ni tarehe ya kuanza kwa vita vya kijeshi huko Tigray, ukatili huo ukiwa ni pamoja na mauaji ya watu wengi, ubakaji, njaa, uharibifu wa shule na vituo vya matibabu, watu kufurushwa kwa lazima na kuwekwa kizuizini kiholela.

Mwenyekiti wa tume hiyo Mohamed Chande Othman amesema machafuko hoivi sasa yako karibu katika kiwango cha kitaifa na yanaainisha ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya raia katika jimbo la Ahmar ana pia ukatili unaoendelea.

Bwana Chande ameonya kuwa “Hali katika majimbo ya Oromia, Ahmara na maeneo mengine ya nchi hiyo ikiwemo mwenendo wa ukiukaji , ukwepaji wa sheria na ongezeko la matumizi ya kijeshi zaidi kwa madai ya ulinzi na usalama na hivyo kuongeza hatari ya ukatili na uhalifu.”

Kuswekwa ndani kiholela Amhara

Tume hiyo ya haki za binadamu kuhusu Ethiopia imesema katika jimbo la Amhara ambako serikali ilitangaza hali yadharura mwezi uliopita , imekuwa ikipokea ripoti za makundi ya watu hasa raia kukamatwa kiholela na angalau kulikuwa na shambulio moja la Ndege zisizo na rubani au drone lililofanywa na serikali.

Pia imeelezwa kwamba maeneo mengi ya mijini yako chini ya amri ya kutotembea hovyo na kutawala kwa amri ya kijeshi bila kuwajali raia.

Tume hiyo imesema mfumo huo mara nyingi huambatana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

“Tunatiwa hofu kubwa na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama jimboni Amhara na kuendelea kuwepo kwa hatari ya vyanzo vya uhalifu mkubwa.”

Kwa mujibu wa tume tohi ya haki za binadamu kuhusu Ethipia mahitaji ya kibinadamu yameongezeka katika jimbo hilo . Mwanzoni mwa wezi Agosti mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO Dkt. Tedros Adhamon Ghebreyesus amesema kwamba “Watu wa Amhara hawawzi kumudu mgogoro mwingine ,akisistiza kwamba watu takriban milioni 2 wanahitaji msaada wa afya na hali imefanywa kuwa mbaya zaidi na wimbi la wakimbizi kutoka Sudan nchi ambayo sasa imeghubikwa na vita.”

Tigray inakabiliwa na zahma ya vizazi na vizazi

Akigeukia upande wa Tigray mjumbe wa tume hiyo Radhika Coomaraswamy ameonya kwamba “Ubakaji na ukatili wa kingono na kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana unaofanywa na vikosi vya Eritrea unaendelea katika jimbo hilo.”

Ameongeza kuwa kuendelea kuwepo kwa vikosi vya Eritrea nchini Ethiopia ni ishara bayana ya kuendeleza será ya ukwepaji wa sheria, lakini pia muendelezo wa kuunga mkono na kuvumilia vitendo hivyo kutoka kwa serikali ya shirikisho.