Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa UNHCR na AIDES warejesha matumaini ya wakimbizi wa Rwanda na Burundi nchini DRC

Mradi wa kazi za Sanaa ambao unasaidia wakimbizi kutoka Burundi na Rwanda kujikimu kimaisha Pamoja na familia zao  nchini DRC.
UN News/Byobe Malenga
Mradi wa kazi za Sanaa ambao unasaidia wakimbizi kutoka Burundi na Rwanda kujikimu kimaisha Pamoja na familia zao nchini DRC.

Msaada wa UNHCR na AIDES warejesha matumaini ya wakimbizi wa Rwanda na Burundi nchini DRC

Msaada wa Kibinadamu

Wakimbizi kutoka nchini Rwanda na Burundi wanaopata hifadhi katika nchi Jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wamepata matumaini mapya ya maisha baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na shirika lisilo la kiserikali ya AIDES kuwawezesha kuanzisha mradi wa kazi za Sanaa ambao unawasidia kujikimu kimaisha Pamoja na familia zao. 

Wakimbizi hao pia wameishukuru serikali ya DRC ambao imekuwa ikikirimu wakimbizi kutoka katika nchi hizo mbili kwa zaidi ya miaka 20 sasa. 

Byobe Malenga mwandishi wetu wa Kinshasa alifunga safari hadi Goma Kivu Kaskazini waliko wakimbizi hao na kuzungumza nao

Soundcloud

Ili kukidhi mahitaji yao, wakimbizi hao wanaoishi Kivu Kaskazini wameanza shughuli tofauti. Baadhi wakijikita na utengenezaji wa vikapu, viti, shanga na mikoba, sabuni, maji ya matunda au juisi, na mafuta ya kupikia, ambavyo kwao ni biashara. 

Na wameitumia fursa ya maonesho ya walinda amani yaliyoambatana na maadhimisho ya hivi karibuni ya siku ya walinda amani kunadi wanachokifanya. 

Uwitonze Furaha, ni mkimbizi wa Rwanda, amepitia mafunzo na leo anatengeneza vikapu ili kukidhi maitaji ya familia yake  nchini DRC.
UN News/Byobe Malenga
Uwitonze Furaha, ni mkimbizi wa Rwanda, amepitia mafunzo na leo anatengeneza vikapu ili kukidhi maitaji ya familia yake nchini DRC.

Uwitonze Furaha, ni mkimbizi wa Rwanda, amepitia mafunzo na leo anatengeneza vikapu ili kukidhi maitaji ya familia yake anasema “ Hiki tuna uza kwa bei ya dola 5, hii ni dola 6, na hii ndogo ni 5 hadi 4,5 waliotusaidia ni UNHCR na AIDES. Walitusaidia sana kufanya kazi za mikono kwakweli hii kazi inanisaidia sana sababu kama nafanya kazi hii watoto hawawezi lala njaa na hata kukosa mavazi. 

Wakimbizi walitumbuiza hadhira katika hafla hii kwa nyimbo na ngoma za kitamaduni. Ili kuonyesha mapenzi na kutambua mchango wa DRC, wacheza densi kutoka kundi la Ubumwe  ikimaanisha Muungano waliamua kuvalia mavazi ya bendera ya DRC badala ya bendera ya Rwanda. 

Shishika Pascasie, ni mkimbizi wa Burundi anatoa shukrani kwa mafunzo aliyopata kutoka UNHCR na kwa sasa ana uwezo wa kutengeneza sabuni, Omo, juisi na vingine nchini DRC.
UN News/Byobe Malenga
Shishika Pascasie, ni mkimbizi wa Burundi anatoa shukrani kwa mafunzo aliyopata kutoka UNHCR na kwa sasa ana uwezo wa kutengeneza sabuni, Omo, juisi na vingine nchini DRC.

Shishika Pascasie, ni mkimbizi wa Burundi anatoa shukrani kwa mafunzo aliyopata kutoka UNHCR na kwa sasa ana uwezo wa kutengeneza sabuni, Omo, juisi na vingine. Nilifika hapa nilikuwa tayari nimesha juwa kazi hii lakini sikuwa na chochote cha kuanzia. Nilipopata msaada wa pesa kutoka kwa UNCHR ndipo sasa nilianza kazi hii. inanisaidia kulipia watoto shule,kula na mavazi pia na kulipia nyumba yangu. mimi naomba wakimbizi wenzetu kujifunza kazi za mikono wasitegemee tu UHCR. Kesho UNHCR inaweza funga milango watabaki wageni wa nani ; Naomba kila mtu ajifunze kazi ya kujitegemea kwa hili tunashukuru UNHCR na kwa wale ambao hawajapata mafunzo sisi ambao tulishajuwa tuwape mafunzo.

Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR mara nyingi huwa hai katika kutoa usaidizi kwa wakimbizi. 

Hii ni pamoja na mafunzo na msaada wa nyenzo. Abdoulaye Barry, mkuu wa ofisi ndogo ya UNHCR Goma, anazungumzia uungwaji mkono wa kamishna wa wakimbizi. Hali ya usalama sio nzuri sana, lakini ningependa kupongeza kwa dhati juhudi za wakimbizi hawa hapa. Licha ya hali hizi ngumu, UNHCR ilichangia katika mafunzo ya baadhi ya wakimbizi hao, hasa katika mafunzo ya ufundi stadi. UNHCR, pia katika sehemu za kuwasaidia baadhi ya wakimbizi hao ilikuwa ni kupitia mchango wa kifedha ili waweze kufanya jambo fulani. 

Mradi wa kazi za Sanaa ambao unasaidia wakimbizi kutoka Burundi na Rwanda kujikimu kimaisha Pamoja na familia zao  nchini DRC.
UN News/Byobe Malenga
Mradi wa kazi za Sanaa ambao unasaidia wakimbizi kutoka Burundi na Rwanda kujikimu kimaisha Pamoja na familia zao nchini DRC.

Benjamin Munege, mratibu wa miradi ya AIDES mashariki mwa DRC, na mshirika wa kiufundi wa NGO ya UNHCR, anasema kuwa lengo la UNHCR ni kuwawezesha wakimbizi ambao wamefaidika na ukarimu wa Wacongo kwa miaka kadhaa, “Kulikuwa na miaka kadhaa hapo awali ambapo mpango wa UNHCR ulifikiria kuwafanya wakimbizi wajitegemee. Wapo baadhi yao walionufaika na fedha za kufanya shughuli za kuwaingizia kipato, na zaidi ya hayo, baadhi yao wapo hapa. Hawa wanaambatana na wenzao wa Congo katika mifumo angalau kutoka kwa uhuru hadi uwezeshaji. Lakini kwa nini wacongo? Kwa sababu Wacongo wanaojenga ni watu wakarimu na kwa nafasi hii angalau, wamerahisisha wenzao wakimbizi kuwarejesha, waandamane nao ili angalau wajichukulie wenyewe. 

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mwaka huu wa 2023, kutokana na kuzuka upya kwa ghasia za kutisha zinazosababishwa na makundi yenye silaha, watu milioni 6.2 wamelazimika kuyahama makazi yao katika majimbo ya Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Tanganyika, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiwa ni nyongeza ya idadi ya wakimbizi 522,000 ambao tayari wako nchini.

Imeandaliwa na Byobe Malenga , DRC.