Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhibiti unahitajika kwa AI  ili kunufaisha kila mtu: Guterres

Maonyesho ya AI katika mkutano wa kimataifa 2023.
© ITU/D.Woldu
Maonyesho ya AI katika mkutano wa kimataifa 2023.

Udhibiti unahitajika kwa AI  ili kunufaisha kila mtu: Guterres

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Uundaji wa akili bandia, au AI, kwa faida ya wote unahitaji njia za ulinzi zinazozingatia haki za binadamu, uwazi na uwajibikaji, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.

Amesisitiza kwamba AI lazima ifaidishe kila mtu, ikiwa ni pamoja na theluthi moja ya binadamu ambao bado hawana huduma ya mtandao, na ameendelea kusisitiza juu ya haja ya kupata maelewano ya haraka kuhusu kanuni zinazoongoza kupelekwa kwa teknolojia ya akili bandia zinapaswa kuwepo.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alikuwa akizungumza hayo katika mkutano wa kilele wa "AI kwa manufaa ya wote" ulioandaliwa mjini Geneva Uswisi na Muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU, ulioleta pamoja serikali, mashirika ya kiraia, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wabunifu wa AI na wawekezaji.

Mkutano huo linachunguza njia ambazo AI inaweza kutumika kusaidia ulimwengu kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs.

Maonyesho ya AI katika Mkutano wa kimataifa 2023.
© ITU/D.Woldu
Maonyesho ya AI katika Mkutano wa kimataifa 2023.

Kurejesha SDG kwenye mstari

Kwa upande wa waandaaji wa mkutano huo ITU Katibu Mkuu Doreen Bogdan-Martin ametoa wito wa ushirikiano wa kimataifa "kuhakikisha AI inafikia uwezo wake kamili, huku ikizuia na kupunguza madhara. Katika hatua ya katikati ya kuelekea tarehe ya mwisho ambayo binadamu wamejipa kufikia SDGs, dunia iko nje ya mkondo wa utekelezaji, “ amesema mkuu huyo wa ITU akiongeza kuwa “kutumia AI kuharakisha maendeleo sasa ni jukumu letu".

Katika hali nzuri, Bi. Bogdan-Martin amesema kuwa “tutaweza kutumia AI kwa mafanikio kupata tiba ya magonjwa kama saratani na Alzeima, kuongeza uzalishaji wa nishati safi na kusaidia wakulima katika kuongeza mavuno ya mazao yao.

Hatari zinazoongezeka za AI 

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo wa ITU ameongeza kuwa “Lakini mustakabali wa hali ya siku za usoni pia unawezekana, ambapo AI inaharibu kazi na kuwezesha kuenea kusikoweza kudhibitiwa kwa taarifa potofu, au ambapo ni nchi tajiri pekee ndizo zilizovuna manufaa ya teknolojia hiyo”.

Mapema mwaka huu, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk alionya juu ya maendeleo ya haraka na yasiyodhibitiwa katika uzalishaji wa AI. 

Alisema "uwakala wa kibinadamu, utu wa binadamu na haki zote za binadamu ziko hatarini", akitoa wito kwa serikali na wafanyabiashara kusisitiza maendeleo ya teknolojia katika kuzingatia masuala ya haki za binadamu.

Zaidi ya roboti 50 zinahudhuria Mkutano wa AI for Good Global Summit 2023.
© ITU/D.Woldu

Fursa ya kihistoria

Mkuu huyo wa ITU amesisitiza kuwa mkutano wa AI unafanyika katika wakati wa kihistoria, wakati ambao ni muhimu kusukuma utawala wa AI na kuhakikisha unakuwa jumuishi, salama na wa kuwajibika.

Ameongeza kuwa mustakabali wa AI bado haujaandikwa

Roboti bunifu

Zaidi ya roboti 50 zitakuwepo kwenye mkutano huo kama sehemu ya maonyesho ya "Roboti kwa manufaa ". 

Wavumbuzi wao wataonyesha jinsi roboti hizo zinavyoweza kusaidia afya ya watu, kutoa huduma za elimu, kusaidia watu wenye ulemavu, kupunguza taka na kusaidia kukabiliana na dharura katika majanga.

Idadi kubwa ya roboti zenye umbo la binadamu zinachukuliwa kama wazungumzaji katika mkutano huo na uwezo wao kama walezi na wasaidizi wa wazee utaonyeshwa.

Mkutano na waandishi wa habari unatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa ambapo baadhi ya roboti hizo za kibinadamu zitakuwa zikijibu maswali.