Skip to main content

Chuja:

Akili bandia

04 AGOSTI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu na Akili Mnemba au ‘Artificial Intelligence’.  Makala tunakupeleka nchini Brazil na mashinani tutasikia ujumbe wa kijana kutoka Tanzania, salía papo hapo!  

Sauti
11'25"
Teknolojia ya droni nayo inaweza kuwa na manufaa bora au hasara kwa kutegemea inatumika kwenye misingi ipi. Hapa ni kwenye maonyesho ya ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu data uliofanyika Dubai 2018
IISD/ENB

Akili Mnemba (AI) ilete nuru na si giza – Katibu Mkuu UN

Hii leo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu amani na usalama duniani likimulika fursa na hatari zitokanazo na Akili Mnemba au Akili Bandia, AI ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesihi Baraza hilo lioneshe uongozi katika nyanja hiyo hasa katika kuhakikisha teknolojia hiyo inatumika kujenga madaraja ya kijamii, kidijitali na kiuchumi badala ya kuleta utengano na uharibifu.

06 JULAI 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Eugene Uwimana mmoja wa maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda amemtembelea mhamasishaji wa lugha ya Kiswahili nchini humo Profesa Pacifique Malonga ambaye ameanzisha eneo maalumu la vitabu vya Kiswahili katika Maktaba Kuu ya mji wa Kigali. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za uhamiaji, usafirishaji haramu wa binadamu na Akili Bandia. Katika jifunze Kiswahili hii leo tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA kupata ujumbe maalum kuhusu umuhimu wa lugha.  

Sauti
12'10"

27 JUNI 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo inaturejesha hapa Makao makuu ya umoja wa Mataifa kusiki maandalizi ya maadhimisho ya pili ya siku ya Lugha ya Kiswahili duniani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu watoto katika migogoro ya silaha, msaada kwa wakimbizi nchini Sudan na maadili ya akili bandia. Katika mashinani tunakupeleka nchini Mali, kulikoni?

Sauti
15'49"

11 Februari 2022

Miongoni mwa yaliyomo 

Kujaa maji kwa ziwa Albert nchini Uganda kwaleta zahma kubwa kwa wakazi, wengine wapoteza makazi, Umoja wa Mataifa nao wanyoosha mkono kusaidia. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres asema kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya viwango vya chini vya wanawake wanaofanya kazi katika masuala ya Akili Bandia (AI), na kanuni za hovyo za upendeleo wa kijinsia. 

Sauti
12'38"