Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa usawa ukizidi kuota mizizi, UN yahaha kuhakikisha kunakuwepo na usawa

Pichani ni Kiara mtoto mwenye umri wa miaka 5 akiuza vibanio vya nywele ndani ya  treni. Kiara amekuwa akifanya biashara hii tangu akiwa na umri wa miaka mitatu.
UNICEF/UNI103753/Rich
Pichani ni Kiara mtoto mwenye umri wa miaka 5 akiuza vibanio vya nywele ndani ya treni. Kiara amekuwa akifanya biashara hii tangu akiwa na umri wa miaka mitatu.

Ukosefu wa usawa ukizidi kuota mizizi, UN yahaha kuhakikisha kunakuwepo na usawa

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs- ni mwongozo wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mustakabali mzuri na endelevu kwa wote- na unatoa wito kwa kuziba pengo la utofauti kati ya nchi na ndani ya nchi. Hatahivyo, ukosefu wa usawa kimataifa unaongezeka. Kwa hiyo ni ni kifanyike?

Ukosefu wa usawa umekita mizizi

Suala la ukosefu wa usawa lilizungumziwa mara nyingi na Umoja wa Mataifa mwezi Janyuari: ambapo akizungumza kwenye jukwaa la kila mwaka la uchumi duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres alisema licha ya kwamba hatua zimepigwa na utandawazi umechangia katika hatua chanya kwa miaka mingi, lakini pia vimeongeza ukosefu wa usawa na kutenga mamilioni ya watu.

Katika barua yake ya kila mwaka, Lise Kingo, Mkurugenzi Mkuu wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kimataifa unaounga mkono sekta binafsi katika juhudi zake kufanya biashara inayozingatia maadili, alitanabaisha kuwa mwaka 2018, kulishuhudiwa, “idadi ndogo ya watu ambao wanaendelea kuwa matajiri wakati mabilioni wengine wanasalia nyuma kwenye umaskini.”

Ukosefu wa usawa, sio tu una ongezeka, kukosekana kwa ulinganifu uliokita miziz,” kwa mujibu wa Richard Kozul-Wright, mtaalam wa utandawazi na mkurugenzi katika Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD.

Katika mahojiano na UN News Bwana Kozul amesema kwamba dhana ya viwango vya juu vya watu wasi na ajira hufunika uwazi kuwa mishahara na mazingira ya kazi hayaimariki, na wakati mishahara haijaongezeka kwa muongo, marupurupu na hisa zimekuwa zikiimarika, na ambapo wamiliki wa hisa wamenufaika. Tamko hilo lilitolewa baada ya kuzinduliwa kwa ripoti ya hali ya uchumi na makadirio mwaka 2019, WESP ambayo ilionyesha tofauti ya ukuaji kati ya nchina ndani ya nchi ambao mara nyingi haufiki unakotakiwa kufika.

Je akili bandia itachukua ajira zetu au itazibadilisha ?

Mshiriki katika tamasha la Marekani la sayansi na uhandisi (2014) akiangalia jukwaani roboti wa kwanza mithili ya binadamu ajulikanaye kama Robonaut 2. wakati huo Roboti huyo (R2) alikuwa ndio kwanza amewekewa miguu mirefu ya kumruhusu kutembea.
NASA/Aubrey Gemignani
Mshiriki katika tamasha la Marekani la sayansi na uhandisi (2014) akiangalia jukwaani roboti wa kwanza mithili ya binadamu ajulikanaye kama Robonaut 2. wakati huo Roboti huyo (R2) alikuwa ndio kwanza amewekewa miguu mirefu ya kumruhusu kutembea.

Mwanzo wa mwaka 2019 uliona mchango wa teknolojia ukilengwa katika dunia ya kazi, na athari zake katika ukosefu wa usawa . Shirika la kazi ulimwenguni, ILO lilizindua ripoti ya aina yake Januari: Kamisheni ya kimatiafa kuhusu mustakabali wa kazi. Utafiti ulibainisha kuwa ubunifu wa teknolojia unatoa ‘fursa nyingi kwa wafanyakazi huku ikionya kuwa, iwapo teknolojia hizo hazitatumika kwa kuzingatia ajenda inayoongozwa na kuwekeza kwa watu, taasisi za kazi na ajira endelevu na zenye hadhi, huenda tukakumbwa na hatari ya kuingia katika dunia ambayo inaongeza pengo la ukosefu wa usawa na yasiyotabirika. ‘

Moja ya ubunifu wa kiteknolojia uliotajwa katika ripoti, moja ambao umeangaziwa na vyombo vya habarii, ni akili bandia (AI). Ripoti kutoka kwa shirika la hakimiliki duniani, WIPO iliyochapishwa mwishoni mwa Januari ulibainisha ongezeko ya maombi ya hataza ya akili bandia, ikiashira kuwa akili bandia huenda ikabadili sehemu zote za maisha ya kila siku mbali ya ulimwengu wa teknolojia

Akili bandia inazua raha na uoga kwa wakati mmoja na kuleta hali ambayo kazi nyingi inafanywa na mashine, huku jamii ikigawanywa mara mbili, ya walio nazo na wengine, watu wasioweza kuajirika na bila matarajio ya kupata kazi.

Hata hivyo Kriti Sharma hana mtazamo huo. Amekuwa akitambuliwa na Umoja wa Mataifa kama kiongozi kijana anayesongesha malengo ya maendeleo, endelevu, SDGs, kwa kuzingatia kazi yake ya kuhakikisha kuwa Akili bandia inasaidia kujenga dunia yenye usawa zaidi na bora zaidi. Anatumia shirika lake la AI For Good yaani Akili bandia kwa maslahi bora, na jukumu lake katika maabara ya Sage Futre Makers ambayo imeanzishwa kusaidia vijana kote duniani kujikita katika kazi zinazohusiana na Akili Bandia, au AI.

Kriti Sharma, Kiongozi Kijana anayesongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.
UN SDGs
Kriti Sharma, Kiongozi Kijana anayesongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa,, Bi. Sharma amekiri kuwa watu wanaoishi kwenye upande wa dunia usio na fursa zaidi ya kupata data au mifumo ya kidijitali, watapata hasara zaidi, na akazungumzia utafiti ambao  unaonyesha tofauti ya kijinsia inayozidi kushamiri, wanawake wakiwa kwenye nafasi ya mara mbili zaidi kupoteza fursa za ajira kutokana na nafasi hizo kuchukuliwa na mashine, na kwa kuzingatia mazingira wanamoishi. “Tunahitaji kuhakikisha kuwa tunawapatia watu fursa sawa ili wajijengee upya stadi, la sivyo tunajenga ukosefu wa usawa kuliko wakati wowote ule.”

Hata hivyo anaamini kuwa moja ya hatari kubwa ya kushindwa kukubali teknolojia hii, na badala yake kutowapatia watu stadi wanazohitaji ili watumie teknolojia  hii kutatua matatizo yanayokumba dunia. Bi. Sharma anataja mambo muhimu matatu ya kuwezesha Akili Bandia inajenga dunia yenye usawa.

Mosi, ni muhimu kwamba watu kutoka makundi mbalimbali wanabuni teknolojia hii, watu ambao wanaelewa jamii na wanaelewa watunga sera. Pili ni kuhakikisha kuwa Akili Bandia inatumika kutatua matatizo sahihi, kama vile kusongesha malengo ya maendeleo endelevu kwa kuelekeza tafiti, fedha na nishati kwenye eneo hilo. Na tatu ni lazima tukubaliane viwango vya kimataifa, kuhakikisha teknolojia tunayobuni ni salama na inazingatia maadili ya duniani.

Hakuna maendeleo bila ushirikiano wa kimataifa

Kwa hiyo, mwelekeo ni  upi basi katika mizania hii isiyokuwa ya usawa kuhusu ukosefu wa usawa? Kwa Umoja wa Mataifa, msisitizo wa ushirikiano wa kimataifa ni muhimu kama suluhu. Ripoti yam waka 2019 kuhusu hali ya uchumi duniani na matarajio imehitimisha kuwa, katika ngazi ya kimataifa, “ushirikiano na mkakati wa muda mrefu wa kisera ndio jawabu mujarabu katika kusongesha harakati za kupunguza ukosefu wa usawa kwenye kipato na ikaonya kuwa “kujiondoa katika ushirikiano wa kimataifa kutaleta hatari zaidi kwa wale ambao tayari wamo ndani ya ushirika huo.”

Kama ambavyo Katibu Mkuu aliwaeleza wajumbe huko Davos kwamba, hatua za kimataifa zilizoratibiwa ni njia pekee ya kutatua ukosefu wa usawa kwasababu “tunapasaw kushirikiana. Haiwezekani mtu mmoja kutatua peke yake matatizo yanayotukabili, kwa kuwa matatizo yote yanaingiliana.”