ITU, Will.i.am, na Google wazindua mafunzo ya AI na roboti kwa vijana barani Afrika
Shirika la Umoja wa Mataifa la Muungano wa Mawasiliano ITU linalohusika na teknolojia za kidijitali, limeungana na mjasiriamali wa teknolojia na mwanamuziki nyota will.i.am pamoja na kampuni ya Google ili kutoa mafunzo ya Akili mnemba AI na roboti kwa wanafunzi barani Afrika.