Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuimarisha huduma za maji safi nakujisafi kutaokoa maisha ya watu mil 1.4 kwa mwaka

UNICEF inaisaidia Serikali ya Malawi katika kutoa maji safi na salama katika kambi zinazowahifadhi manusura wa kimbunga Freddy.
© UNICEF/Thoko Chikondi
UNICEF inaisaidia Serikali ya Malawi katika kutoa maji safi na salama katika kambi zinazowahifadhi manusura wa kimbunga Freddy.

Kuimarisha huduma za maji safi nakujisafi kutaokoa maisha ya watu mil 1.4 kwa mwaka

Afya

Ingawa huduma za maji safi na kujisafi zimeongezeka katika kipindi cha miaka 10 lakini bado maendeleo hayo ni madogo na hayatoshi kupambana na athari zinazoletwa na ukosefu wa huduma hiyo muhimu imesema ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO na kuchapishwa na jarida la The Lancet. 

Ripoti hiyo imebainisha kuwa nusu ya idadi ya watu ulimwenguni bado hawana huduma ya kutosha ya maji safi ya kunywa, kujisafi na usafi wa mazingira (WASH) na iwapo idadi hiyo ya watu ingeweza kupata huduma hiyo ingeweza kuzuia vifo vya watu milioni 1.4. 

“Kuendelea kuongezeka kwa magonjwa yasababishwayo na WASH kutokana na mizozo, hatari za viua vijiumbe maradhi, hatari za kuibuka kwa magojwa ya kipindupindu na athari za muda mredu ziletwazo na athari za mabadiliko ya tabianchi zote hizi zinaonesha hitaji la haraka la uwekezaji.” Amesema Dkt.Maria Neira Mkuu wa Idara ya Mazingira, tabianchi na afya wa WHO

Ripoti hiyo imeeleza pia mzigo wa magonjwa ulioletwa na ukosefu wa maji safi, kujisafi na huduma za kujisafi kwa nchi 183 wanachama wa WHO zikitanabaisha maeneo, umri na jinsia kwa mwaka wa 2019.

Magonjwa

Magonjwa makuu manne ni kuharisha, changamoto za kupumua, utapiamlo, na ugonjwa wa helminthiases unaoenezwa kupitia udongo. 

Ugonjwa wa kuharisha umeelezwa kusababisha vifo vya watu milioni 55 kila siku ukifuatiwa na matatizo ya kupumua unaogharimu maisha ya watu milioni 17 kila siku. 

Miongoni mwa watoto walio chini ya miaka mitano, magonjwa yatonakanayo na shida ya majo yamesababisha vifo 395,000 sawa na  kila siku watoto milioni 37, ikiwakilisha 7.6% ya vifo vyote na 7.5% ya DALY zote katika kikundi hiki cha umri. Hii ilijumuisha vifo 273,000 kutokana na kuhara na vifo 112,000 kutokana na magonjwa ya kupumua kwa papo hapo. Magonjwa haya ndio sababu kuu mbili za kuambukiza za vifo vya watoto chini ya miaka mitano ulimwenguni.

Kanda zinatofautiana kwa kuathirika

Tofauti muhimu zilibainishwa kati ripoti hiyo ni kulingana na kanda na kipato cha nchi. 

Zaidi ya robo tatu ya vifo vyote vilivyotokana na changamoto za WASH vilitokea katika kanda za WHO za Afrika na Kusini-Mashariki mwa bara la Asia. 

Pia asilimia 89 za vifo vilivyotokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati. Hata hivyo, nchi zenye kipato cha juu ziko hatarini, kwani asilimia 18 magonjwa ya kuharisha yanaweza kuzuiwa kupitia njia bora za usafi wa mikono. 

Nini kifanyike

Ili kupunguza magonjwa haya Who imependekeza masuala kadhaa ambayo nchi zinapaswa kufanya kwa kushirikiana na msaada wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, wadau wengine wa maendeleo, sekta binafsi na asasi za kiraia. 

Masuala hayo ni pamoja na mosi, kuhakikisha maeneo yote watu wanapata maji safi ya kujisafi, pili, kuweka mkazi zaidi katika maeneo ya watu masikini na wasiojiweza, na tatu kuweka mifumo ya kitaifa ya kufuatilia takwimu za idadi ya watu na huduma zinazotolewa ili kufuatilia kwa karibu na kuhakikisha wananchi wako salama.

“Ni dhahiri ukosefu wa upatikanaji wa maji safi, huduma za kujisafi na huduma nyingine za usafi unaendelea kusababisha hatari kubwa, na inayoweza kuzuilika, ya kiafya, haswa kwa watu walio hatarini zaidi," alisema Bw. Bruce Gordon, Mkuu wa WHO kutoka idara ya Maji, Usafi wa Mazingira, Usafi na Kitengo cha Afya.

Gordon ameongeza kuwa faida za kiafya, kama ilivyobainishwa katika ripoti, ni kubwa. “Kutanguliza wale wanaohitaji zaidi sio tu sharti la kimaadili ni muhimu katika kukabiliana na mzigo usio na uwiano wa magonjwa katika nchi za kipato cha chini na cha kati na miongoni mwa makundi yaliyotengwa katika nchi za kipato cha juu.”

Katika kuunga mkono juhudi za serikalli kupamba na  magonjw ahayo WHO leo imetoa zana mpya ya kuonesha athari ziletwazo na magonjw ayasababishwayo na WASH. Zana hii itasaidia katika utungaji wa será wakati nchi tayari ina ufahamu wa hali ilivyo, kuw ana muongozo wa nini kinapswa kufanyika, na kusaidia ugawaji wa rasilimali za kimkakati kwa ajili ya programu ya usafi na kujisafi.

Kusoma zaidi ripoti hii bofya hapa .