Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti 3 zaonesha athari wanazokabiliana nazo watoto wa Rohinghya

Mama akiwa amembeba mwanae wakati wakiwasili fukwe ya Dakhinpara, nchini Bangladesh wakitokea Myanmar. © UNHCR/Adam Dean

Ripoti 3 zaonesha athari wanazokabiliana nazo watoto wa Rohinghya

Utapiamlo uliokithiri, upungufu wa damu na kipindupindu vyawakumba watoto wadogo wa kabila la Rhohingya waliokimbilia nchini Bangladesh.

Ripoti tatu maalum za shirika la kuhudumia watoto ulimwenguni UNICEF zinasema katika kila watoto 5,  wawili kati yao wanaugua kipindupindu, na mmoja kati ya 5 ana utapiamlo uliokithiri huku  mmoja kati ya 2 ana upungufu wa damu.

Mwakilishi wa UNICEF Bangladesh Edouard Beigbeder, ametaka juhudi za haraka zifanyike kuokoa watoto hao

(Sauti ya Edouard  Beigbeder)

“Mashirika ya misaada yaliyopo hapa yameshajitahidi sana kupambana na hali inayosumbua watoto pamoja na utapiamlo, lakini juhudi hizi lazima ziongezeke ili kuhakikisha watoto hawa wanapata mlo kamili, maji safi na salama na huduma za afya”

Watoto hao wa kabila la Rohingya pamoja na familia zao walikimbilia nchini Bangladesh kusaka hifadhi mara baada ya kuzuka kwa mapigano nchini mwao Myanmar mwezi Agosti mwaka huu.