WASH

Maji ya kunawa mikono majumbani bado ni shida kwa mabilioni ya watu duniani

Takwimu mpya zinaonesha kuwa watu 3 kati ya 10 duniani kote hawakuweza kuosha mikono yao kwa maji na sabuni wakiwa nyumbani wakati wa janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.
 

UNICEF Zambia yatumia WASH kunusuru wakimbizi na wenyeji

Nchini Zambia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia jimbo la Luapula lililoko mpakani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kuwa na huduma za kujisafi na maji safi, WASH kwa lengo la kuondokana na magonjwa ya kuambukiza na pia kupatia watoto fursa ya kutosha ya kujifunza.

25 Januari 2021

Hii leo mwenyeji wako Grace Kaneiya akiwa Nairobi Kenya anajikita katika mada kwa kina kutoka Zambia ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,

Sauti -
10'27"

Takriban watu bilioni 2 wanategemea vituo vya afya visivyo na huduma ya WASH:UNICEF/WHO

Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto duniani UNICEF la afya WHO leo yameonya kwamba ukosefu wa maji katika vituo vya huduma za afya unawaweka wafanyakazi na wagonjwa katika hatari kubwa ya maambukizi ya corona au COVID-19.

Asante UNICEF kwa kutusaidia wakati huu wa mafuriko:Waathirika Kenya  

Waathirika wa mafuriko makubwa yanayokumba maeneo mbalimbali ya Mashariki mwa Afrika na kusababisha athari  ikiwemo watu kupoteza kila kitu, hususan  nchini Kenya wamelishukuru shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kuwasaidia. 

Shule zikiwa zinaanza kufunguliwa, bado hakuna huduma za kujisafi kujikinga na COVID-19- Ripoti

Mjini Mangina jimboni Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mtaalamu wa mradi wa huduma za maji, kujisafi na kunawa mikono, WASH kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto

Sauti -
2'53"

Kupambana na COVID-19 maji si uhai tu ni lazima:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema katika kupambana na janga la virusi vya corona au COVID-19 ni muhimu kuhakikisha kila mtu anapata huduma ya maji ambayo si uhai tu bali ni lazima

Kituo kimoja cha afya kati ya vinne hakina huduma ya maji-UNICEF/WHO.

Kati ya vituo vinne vya afya duniani kote, kimoja kinakosa huduma za maji, hali inayowaathiri zaidi ya watu bilioni mbili. John kibego na taarifa kamili. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya pamoja iliyotolewa usiku wa kuamkia leo mjini Geneva Uswisi na New York Marekani na shirika la afya duniani WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Ripoti maalum yasema shule nyingi duniani hazina maji safi na salama ya kunywa

Wiki ya maji ikiwa inaendelea kuadhimishwa kote duniani, inaelezwa kuwa asilimia 69 ya shule ulimwenguni kote hazina huduma ya maji ya kunywa, imesema ripoti ya kwanza ya mashirika ya Umoja wa Mataifa iliyoangazia makadirio ya upatikanaji wa maji ya kunywa, huduma za kujisafi na

Sauti -
1'50"

Maji yakiwa jirani watoto wana muda wa kusoma na kucheza

Suluba ya kutembea muda mrefu wakati akiwa mtoto ili kutafuta maji ilikuwa ni kichocheo kwa kijana mmoja huko Sudan Kusini kuamua kusoma uhandisi na sasa amefanikisha kujengea jamii yake mfumo endelevu wa maji safi na salama.