Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa maandalizi wa operesheni za wanawake katika ulinzi wa amani umeng’oa nanga Dhaka

Wanawake walindamani wa Ghana wakiwa wamepelekwa Lebanon kama sehemu ya operesheni ya ulinzi wa amani ya UNIFIL
UNIFIL/Pasqual Gorriz
Wanawake walindamani wa Ghana wakiwa wamepelekwa Lebanon kama sehemu ya operesheni ya ulinzi wa amani ya UNIFIL

Mkutano wa maandalizi wa operesheni za wanawake katika ulinzi wa amani umeng’oa nanga Dhaka

Amani na Usalama

Mkutano wa kimataifa wa maandalizi ya operesheni za wanawake katika ulinzi wa amani leo umefungua pazia mjini Dhaka Bangladesh.

Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na serikali za Bangladesh ambayo ndio mwenyeji, Canada na Uruguay ambazo zitawakaribisha washiriki kutoka kila pembe ya dunia kwa kwenye mkutano huo wa kwanza wa maandalizi ya mkutano wa ngazi ya mawaziri wa operesjeni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2023 (UNPKM) ulio chini ya uongozi wa Ghana.

Maudhui ya mkutano huo ni “Wanawake katika ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa.”

Wawakilishi kutoka nchi wachangiaji wa askari na polisi katika ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa , wataalam wa masuala ya ulinzi wa amani katika nhgazi ya wakurugenzi na wakurugenzi wakuu wanahudhuria ili kujadili hatua zilizopigwa, changamoto na kubadilishana uzoefu mzuri katika kuongeza ushiriki wenye tija wa wanawake katika ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa na pia kupanga njia ya kuendelea kuwekeza katika na kusaidia utekelezaji wa mkakati wa usawa wa kijinsia uliofanana (UGPS) na utekelezaji wa azimio namba 2538 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake katika ulinzi wa amani (2020), na kuandaa ahadi madhubuti kukabili vikwazo na vizuizi vinavyowakumba walinda amani wanawake wanaovalia sare .

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa  Jean-Pierre Lacroix, amewasili Dhaka, Bangladesh ili kuhudhuria mkutano huu wa kwanza wa maandalizi ya operesheni za ulinzi wa amani wa ngazi ya mawaziri kabla ya mkutano wa mawaziri utakaofanyika Accra, Ghana, tarehe 5 na 6 Desemba 2023.