Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna kinachomshinda mwanamke anapodhamiria:Meja Owuor 

Meja Veronica Owuor, mlinzi wa amani na afisa mafunzo ya kijeshi kwenye operesheni za amani za Umoja wa Mataifa.
UN News/Grece Kaneiya
Meja Veronica Owuor, mlinzi wa amani na afisa mafunzo ya kijeshi kwenye operesheni za amani za Umoja wa Mataifa.

Hakuna kinachomshinda mwanamke anapodhamiria:Meja Owuor 

Amani na Usalama

Kutana na mwanamke shupavu, mlinzi wa amani na afisa mafunzo ya kijeshi kwenye operesheni za amani za Umoja wa Mataifa.

Meja Veronica Owuor ambaye ni afisa wa ununuzi na masuala ya kiufundi katika jeshi la anga la Kenya , lakini kwas asa ni miongoni mwa wanawake wawili tu na pekee kutoka barani Afrika wanaofanyakazi katika idara ya maafisa wa mafunzo ya kijeshi kwenye Umoja wa Mataifa.

Alipotutembelea katika ofisi zetu za UN News kwenye ghorofa ya 11 makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani alipata fursa ya kukutana na wafanyakazi wa lugha mbalimbali waliokuwa na hamasa kubwa ya kujua anachokifanya.

Na ndipo nikaambayana naye Meja veronica na kuketi katika mazungumzo ambapo amenieleza ni kwa nini aliipenda sana kazi hii ya jeshi na kutoa mafunzo, "Kazi hii nilipenda kwa sababu baba yangu ambaye amestaafu alikuwa polisi kwa hiyo nilipenda kuchukua sare yake na fimbo yake pia katika kazi hii ambayo ninafanya katika Umoja wa Mataifa ya kutoa mafunzo, mama yangu ambaye kwa sasa amestaafu alikuwa ni mwalimu kwa hiyo nimerithi hiyo ari ya kuwa jeshi na kuwa mwalimu. Nahusika na kutengeneza mtaala na kutoa mafunzo katika nchi mbali mbali  na kutathimini kama nchi zinazingatia muongozo wa Umoja wa Mataifa."

Nimemuuliza Meja Veronica ni changamoto gani kama mwanamke anayefunza idadi kubwa ya wanaume kwenye operesheni za ulinzi amani anakumbana nazo, "changamoto kubwa ni kujaribu kuhimiza nchi kwamba wanawake pia wanaweza kazi hizi za Umoja wa Mataifa, kwa sababu unapata kwamba nchi nyingi zina changamoto katika kujumuisha wanawake katika operesheni kwa sababu dhana ni kwamba kazi hizi zinahitaji kutumia nguvu lakini kuna kazi mbali mbali ikiwemo kusaidia raia ambao wako katika maeneo yanayohitaji ulinzi."