Njia 5 za ushirikiano zinazotumiwa na Walinda Amani  zinazochangia kuleta amani na maendeleo

29 Mei 2022

Kila siku, walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanafanya kazi ili kuwalinda mamilioni ya watu walio hatarini katika maeneo hatarishi yanayozidi kuwa katika mazingira tete ya kisiasa duniani.

Kuanzia kulinda raia katika maeneo yenye vita na kujenga mshikamano wa kijamii, hadi kuhakikisha uwasilishaji salama wa misaada ya kibinadamu, kujenga upya miundombinu, na kutoa stadi za kujikimu na maisha kwa jamii maskini - walinda amani hufanya kazi na washirika wa ndani ya nchi wanazolinda amani a kimataifa ili kusaidia kuweka mazingira yatakayo leta suluhu za kisiasa na maendeleo endelevu.

Katika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa ambayo huadhimishwa kila mwaka Mei 29 ambayo Kauli mbiu mwaka huu ni Maendeleo ya Amani ya Watu: Nguvu ya Ushirikiano, hizi ni njia tano za ushirikiano wa kulinda amani huleta mabadiliko.

Eneo la Unity nchini SUdan Kusini lilikabiliwa na mafuriko mabaya kabisa katika kipindi cha miaka 60 mnamo Disemba 2021.
UNMISS
Eneo la Unity nchini SUdan Kusini lilikabiliwa na mafuriko mabaya kabisa katika kipindi cha miaka 60 mnamo Disemba 2021.
  1. Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya tabianchi huongeza hatari ya mzozo na hufanya maridhiano kuwa ngumu zaidi. Kuongezeka kwa ukame, kuenea kwa jangwa, mafuriko, uhaba wa chakula, na uhaba wa maji na nishati katika sehemu nyingi za dunia, kunafanya iwe vigumu kwa jumuiya zilizoathiriwa na migogoro kujenga upya maisha yao.

Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa unahudumu na kuwa mstari wa mbele wa kuleta suluhisho za migogoro hii.

UNMISS, Sudan Kusini: Mapambano ya kutatua changamoto ya maji

Mnamo mwezi Disemba 2021, asilimia 70 ya eneo la muungano la Sudan Kusini lilifunikwa na maji, kufuatia mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutoka katika kipindi cha miaka 60.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), kwa ushirikiano na wadau wa misaada ya kibinadamu na mamlaka za maeneo za maeneo yaliyoathirika, ulichukua hatua mara moja, na wahandisi wa kulinda amani kutoka Pakistan wakijenga kilomita 70 za mifereji kulinda mji, kambi za familia zilizopoteza makazi, uwanja wa ndege na barabara zinategemewa katika jukumu muhimu za kusambaza misaada ya kibinadamu pamoja na biashara.

Mnamo tarehe 4 Januari 2022, UNMISS na washirika wake waliadhimisha siku 100 mfululizo za kupambana na maji kufurika. Katika kufanya kazi kwa kushirikiana, jamii za maeneo hayo zilihamasishwa kuendelea kufuatilia  na kuangalia iwapo kuna nyufa katika mifereji ya mirefu ya matope iliyojengwa ili kuzuia maji.

Akitafakari juu ya juhudi hizo kubwa zilizofanyika kwa ushirikiano wa wadau wote Mkuu wa Ofisi ya UNMISS huko Bentiu, Hiroko Hirahara alieleza, "Ninachoweza kuwaambia kwa fahari ni kwamba kila mtu alikuja pamoja. Namaanisha, huu ndio uzuri wa watu wa Bentiu ambao tunaweza kuwa tunagombana hapa, kule, kila mahali, lakini mara tu hali inapotokea, kila mtu huja pamoja. Tunafanya kazi kwa mshikamano. Nadhani tunapiga hatua.”

Mtangazaji wa Radio Okapi, Jody Nkashama.
MONUSCO
Mtangazaji wa Radio Okapi, Jody Nkashama.
  1. Mstari wa mbele katika mapambano ya janga la COVID-19

Tangu kuanza kwa janga la COVID-19, walinda amani wameendelea kuwalinda raia dhidi ya ghasia na kudumisha amani, huku pia wakiunga mkono juhudi za kitaifa za kupambana na janga hilo.

MONUSCO, DR Congo: Mapambano na taarifa potofu

Katika kipindi chote cha janga hili, redio imekuwa njia muhimu ya kusambaza taarifa kwa wakati na sahihi kuhusu maambukizi ya COVID-19, kinga, matibabu na mbinu bora zaidi, hasa katika jamii. Wakati ambapo watu wengi walikuwa wakifanya kazi majumbani kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya wagonjwa wapya wa COVID-19, mtangazaji wa Radio Okapi ya MONUSCO, Jody Nkashama, alikuwa studio, akijaribu kuzuia kuenea ugonjwa huo  kwa kuwafahamisha wasikilizaji mambo mbalimbali.

"Tulijitolea kuhudumia wasikilizaji zaidi ya milioni 24 kwa habari za uhakika juu ya janga hili, ambalo lilizua minong'ono mbalimbali, kupoteza maisha, na kuathiri uchumi wa taifa," ameeleza Nkashama.

Zaidi ya kutoa taarifa za kuokoa maisha na kupambana na upotoshaji hatari kuhusu virusi, Radio Okapi, ambayo inaendeshwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO), ilichukua  jukumu muhimu la kuelimisha wanafunzi wadogo. Huku mamilioni ya watoto wakishindwa kuhudhuria shule kutokana na maagizo ya kukaa nyumbani, Redio Okapi iliingia ili kuziba pengo hilo.

Nchini Sudan Kusini mifugo na tegemeo kw afamilia na huwasidia kupata mahitaji yao.
UNMISS
Nchini Sudan Kusini mifugo na tegemeo kw afamilia na huwasidia kupata mahitaji yao.
  1. Kusaidia maisha ya jamii

Ili amani idumu, jamii zilizoathiriwa na migogoro lazima ziungwe mkono ili kujenga upya mbinu za kujitafutia riziki. Walinzi wa amani hutoa na kufadhili warsha na huduma za mafunzo ya ufundi stadi na ujuzi ili kusaidia jumuiya za wenyeji kuzalisha mapato ambayo yatawawezesha kusaidia familia zao.

UNMISS, Sudan Kusini: Mifugo kama njia ya kuokoa maisha

Nchini Sudan Kusini, mifugo yenye afya nzuri sio tu ishara ya heshima kwa jamii, lakini pia njia ya kuendesha maisha kwa familia nyingi, kuwasaidia kuweka chakula mezani, kukidhi mahitaji ya lishe na kusomesha watoto wao.

Kliniki ya kila wiki ya mifugo ni utamaduni wa muda mrefu huko Malakal, Sudan Kusini, shukrani kwa walinda amani wa India wanaohudumu na Misheni ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS).

Kuanzia mwaka 2006-2015, na kisha 2018, baada ya utulivu wakati wa vita vilivyokithiri katika eneo hilo, walinda amani wa India walitoa huduma za bure za mifugo na mafunzo kwa wakulima wa ndani ili kuhakikisha afya ya mifugo yao.

Bila ya kuwepo kwa madaktari wengine wa mifugo wanaotibu wanyama huko Malakal, huduma za mifugo zilizotolewa na UNMISS ziliokoa maisha ya mifugo na chanzo cha mapato ya wananchi.

"Kusaidia watu kuendeleza maisha yao kunasaidia sana katika kuchangia juhudi za kujenga amani katika taifa hili changa," anasema Lt-Col. Phillip Varghese.

  1. Kujenga uwezo wa kitaifa ili kudumisha amani na usalama

Misheni za ulinzi wa amani hufanya kazi na serikali mwenyeji kujenga na kuboresha uwezo wa kitaifa ili kudumisha usalama, sheria na utulivu, na mifumo madhubuti ya polisi na haki.

Mlinda amani wa MINUSCA akiwa katika doria nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR-Kutoka Maktaba
MINUSCA/Herve Cyriauqe Serefi
Mlinda amani wa MINUSCA akiwa katika doria nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR-Kutoka Maktaba

 

MINUSCA, Jamhuri ya Afrika ya Kati: Kuruhusu amani itawale

Mnamo mwezi Machi 2022, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), ulianzisha operesheni iliyopewa jina "Zia siriri ni Akomandé", (" Amani itawale ") kaskazini magharibi mwa nchi.

Operesheni hiyo inalenga kupunguza ushawishi wa makundi haramu yenye silaha na athari za vifaa vya vilipuzi kupitia kuongezeka kwa doria na uchunguzi wa angani.

Wakifanya kazi kwa karibu na jumuiya za wenyeji na jeshi la taifa, walinda amani hufanya doria kutathmini hali ya usalama na pia kujifunza kuhusu wasiwasi wa jumuiya za wenyeji. Wakati wa doria za hivi majuzi, jamii zilieleza changamoto wanazokabiliana nazo ni ukosefu wa vifaa vya matibabu na ufikiaji wa shule.

Katika kukabiliana na hali hiyo, walinda amani wametoa maji safi ya kunywa kila siku, vifaa vya shule na vifaa vya michezo, pamoja na msaada wa matibabu bila malipo, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto. Barabara pia zimefanyiwa ukarabati ili kuboresha hali ya maisha na upatikanaji wa huduma.

"Idadi ya matukio na mashambulizi katika eneo hilo imepungua kwa kiasi kikubwa katika wiki chache zilizopita, ushahidi kwamba kuna matokeo chanya halisi kutoka kwa vitendo tulivyofanya," kauli ya Lt-Col. Abdoul Aziz Ouédraogo.

5. Kusaidia wanawake na vijana katika kujenga amani endelevu

Uongozi wa wanawake na vijana ni muhimu katika kuunda suluhu zinazoathiri maisha na kuleta amani na maendeleo. Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa zinaunga mkono ushiriki wenye tija wa wanawake na vijana ili kuhakikisha kwamba vipaumbele vyao ni muhimu kwa usalama na maamuzi ya kisiasa.

 

UNFICYP, Kupro: Kutoka kuwa wageni hadi marafiki

Miongo kadhaa ya migogoro imegawanya jamii za Kigiriki na Kituruki za Cyprus. Mnamo mwaka 2021, mradi uliowezeshwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Cyprus (UNFICYP), na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uholanzi, ulisaidia kuwaleta wanawake kutoka jumuiya zote mbili pamoja, kupitia utamaduni wa karne nyingi: kusuka.

Mradi wa Wanawake wa Klotho unaotumia mbinu za asili za kutengeneza nyuzi za asili uliruhusu wanawake wa Cyprus wa Ugiriki na Kituruki wa umri tofauti kubadilishana ujuzi wao wa kusuka nyuzi hizo.

"Mwanzoni, tulihisi kama wageni, lakini kupitia ushirikiano huu wa jumuiya mbili tulipata kujua kwamba sisi ni sawa," anaelezea Hande Toycan, raia wa Kituruki. "Kwa kukutana na kila mmoja wetu, kujua maisha na tabia za kila mmoja wetu, polepole tutafungua njia ya amani."

"Hadi wakati huu, sikuwasiliana hata kidogo na Wa cyprus wa Kituruki," asema Mgiriki wa Cyprus Flora Hadjigeorgiou. "Mara ya kwanza nilipokutana na mturuki wa Cyprus ilikuwa kupitia mradi wa Klotho. Nikiwa na umri wa miaka 65."

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter