Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu saba wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi Jerusalem:UN

Sinagogi la The Haram al Sharif/Temple Mount mjini Jerusalem
Flickr/Tony Kane
Sinagogi la The Haram al Sharif/Temple Mount mjini Jerusalem

Watu saba wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi Jerusalem:UN

Amani na Usalama

Shambulio la kigaidi lililotelkezwa na mshambuliaji wa Kipalestna nje ya synagogue mjini Jerusalem hii leo limekatili maisha ya watu sab ana kujeruhi wengine kadhaa ,na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali shambulio hilo.

Katika taarifa kupitia msemaji wake iliyotolewa jioni ya leo mjini New York Marekani Antonio Guterres ametuma salam za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio hilo na kuwatakia ahuweni ya haraka majeruhi.

Katibu Mkuu amesema “ Ni jambo la kuchukiza sana kwamba shambulio hilo limetokea mahali pa ibada, na siku ambayo tunadhimisha siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya maangamizi makubwa ya Wayahudi. Kamwe hakuna kisingizio chochote cha vitendo vya ugaidi. Lazima vilaaniwe waziwazi na kukataliwa na watu wote.”

Bwana Guterres ameongeza kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa ghasia nchini Israel na ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 

“Huu ni wakati wa kujizuia kabisa na machafuko zaidi”.

Duru za habari zinasema raia hao wa Israel walipoteza maisha baada ya mtu aliyejihami kwa bunduki kuwafyatulia risasi waumini katika sinagogi mjini Jerusalem katika tukio ambalo maafisa wa polisi wanalielezea kama shambulio la kigaidi.

Mshambuliaji huyo, ambaye mamlaka ilimtambua kama mwanamume wa Kipalestina kutoka Jerusalem Mashariki, pia aliuawa na polisi.