UNRWA yaomba dola milioni 38 kwa ajili ya Gaza na Ukingo wa Magharibi 

19 Mei 2021

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko kubwa la vurugu katika eneo linalokaliwa la Wapalestina (oPt) ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uhasama unaosababisha mashambulio makubwa ya anga ya Israeli huko Gaza, ambayo yalianza tarehe 10 Mei mwaka huu wa 2021 na mapigano katika Ukingo wa Magharibi, pamoja na Mashariki mwa Jerusalem na hiyo kulazimu upelekaji wa misaada ya dharura kama linavyofanya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA. 

Katika ombi hili la sasa, UNRWA inatafuta kwa haraka Dola za Kimarekani milioni 38. Kiasi hiki cha pesa kinahitajika ili kutatua mahitaji ya chakula cha haraka, mahitaji mengine yasiyo chakula, afya, msaada wa kisaikolojia, usafi na kujisafi na mahitaji mengine ya kukuza uwezo wa kuchukua hatua muhimu za dharura wakati wa uhasama katika ukanda wa Gaza. 

Shughuli hizi ni kwa ajili ya kutoa msaada wa dharura katika siku 30 tangu kuongezeka kwa mashambulizi mnamo Meo 10 na kusaidia hadi hadi watu 50,000 wanaotafuta usalama. Hii inawakilisha karibu asilimia hamsini ya mipango ya dharura ya kujiandaa kwa dharura.  

“UNRWA inafuatilia hali hiyo kila wakati na itaboresha tathmini yake ya mahitaji kulingana na hali. Mahitaji ya kurejea haraka katika hali ya zamani na ujenzi hayajaonyeshwa katika ombi hili la dharura.” Imesema taarifa hiyo.  

Huko Gaza, UNRWA tayari imekuwa ikitoa msaada wa mahitaji ya kibinadamu ya watu walioathiriwa wakiwemo  wakimbizi na wasio wakimbizi, pamoja na maelfu ya watu ambao wametafuta usalama katika shule za UNRWA huko Gaza pamoja na Makazi ya Dharura, DESs ambayo yamewekwa kuwa hifadhi ya wakimbizi wa ndani, IDPs wakati wa mizozo. 

Ombi hili pia linajumuisha sehemu ya mahitaji ya dharura katika Ukingo wa Magharibi, pamoja na Mashariki mwa Yerusalemu, katika sekta za afya, makazi, elimu, usalama na ulinzi, ambapo mahitaji yameongezeka kutokana na mivutano inayoongezeka. 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter