Skip to main content

kupokonya raslimali za wapalestina, ni ukiukaji wa haki za binadamu-Mtaalamu wa UN

Mwakilishi wa UNmkuhusu hali ya haki za binadamu kwa eneo linalokaliwa la Palestina tangu mwaka 1967 Michael Lynk akizungumza na waandichi wa habari mjini Geneva Uswis.
PICHA na UN/Kim Haungton
Mwakilishi wa UNmkuhusu hali ya haki za binadamu kwa eneo linalokaliwa la Palestina tangu mwaka 1967 Michael Lynk akizungumza na waandichi wa habari mjini Geneva Uswis.

kupokonya raslimali za wapalestina, ni ukiukaji wa haki za binadamu-Mtaalamu wa UN

Haki za binadamu

Mwakilishi maalumu wa Umoha wa Mataifa kuhusu haki za rasilimali  , Michael Lynk hii leo mjini Geneva Uswisi amesema upokonyaji wa raslimali za wapalestina unaofanywa na Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa ni ukiukwaji wa moja kwa moja wa wajiu wa kisheria.

Bwana Lynk akiwasilisha ripoti yake kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa amesema, “kwa takribani wapalestina milioni 5 wanaoishi katika eneo linalokaliwa, kuharibiwa kwa vyanzo vyao vya maji, kupokonywa kwa maliasili zao na kuharibu mazingira yao, ni dalili ya dhahiri ya ukosefu wa udhibiti wa namna yoyote wa maisha yao ya kila siku.”

Aidha bwana Lynk ameongeza kusema, “sera za Israel za kutwaa maeneo ya maliasili ya wapalestina na kuharibu mazingira, imechukua mali muhimu ya wapalestina na hiyo inawanyima fursa yao ya kufurahia haki ya maendeleo.”

Ripoti ya Lynk ambayo imejikita katika kitendo cha Israel kulikalia eneo la Palestina kwa upande wa mazingira na maliasili, imesema watu wanaoishi katika eneo linalokaliwa wanastahili kufurahia haki za binadamu kikamilifu kama zinavyotamkwa katika sheria za kimataifa ili kulinda umoja wao juu ya utajiri wao wa asili.

Mtaalamu huyo amesema utajiri wa asili na madini katika ukingo wa magharibi unavunwa na Israel kwa manuafaa yao wakati wapalestina wanazuiliwa.

Pia kuna malalamiko kuwa Israel imekuwa ikimwaga taka zenye sumu katika maeneo ya ukingo wa Magharibi. Matokeo ya matendo hayo yanaweza kuwadhuru siyo tu wapalestina bali pia waisrael na watu wengine katika ukanda huo, amesema mtaalamu wa Umoja wa Mataifa.

Ripoti pia imezungumzia matumizi ya nguvu nyingi yanayofanywa na Israel dhidi ya waandamanaji. Pia bwana Lynk ameeleza hofu yake kuhusu mustakabali wa familia takribani 200 za wapalestina walioko Jerusalemu Mashariki ambao wako katika hatari ya kufurushwa.