Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka wazo la darasani mpaka Kampuni : Digital Kiota

Mtoto wa umri wa miaka 11 akijisomea kitabu chake cha darasa la sita nyumbani mjini Nairobi Kenya. Haziwezi kushiriki katika masomo ya mtandaoni kwa kuwa familia yake haina simu ya mkononi.
© UNICEF/Everett
Mtoto wa umri wa miaka 11 akijisomea kitabu chake cha darasa la sita nyumbani mjini Nairobi Kenya. Haziwezi kushiriki katika masomo ya mtandaoni kwa kuwa familia yake haina simu ya mkononi.

Kutoka wazo la darasani mpaka Kampuni : Digital Kiota

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Janga la COVID 19 lilipotangazwa mwaka 2019 lilizua taharuki kila kona ya dunia lakini changamoto zilizoletwa na janga hilo zilikuwa fursa kwa vijana nchini Zimbabwe ambao walikuja na wazo la shule mtandaoni na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeo UNDP likawapa fedha ili watekeleze wazo na kuwanufaisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. 

Kudakwashe Mlambo, mwazilishi wa Kampuni ya Digital kiota, kampuni ambayo miongoni mwa kazi zake wana jukwaa liitwalo cheza na ujifunze ambayo kupitia video ya UN anasema “Kimsingi ni jukwaa, la kujifunza mtandaoni ambalo lina maudhui ya video yaliyorekodiwa awali na yanafuata muongozi wa mtaala wa Zimbabwe kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.”

Anasema katika jukwaa hilo wana walimu ambao wanarekodi masomo na pembeni ya video ya mwalimu kunakuwa na picha au michoro inayoonesha kile mwalimu anachofundisha ili kujenga uelewa zaidi.

Mlambo anasema wazo la jukwaa hili alilipata akiwa chuoni wakati wakijadiliana na wenzake lakini hakuwa na uwezo wakifedha wala kiufundi wa kulitekeleza kwa wakati huo lakini baada ya kusikia tangazo la UNDP kuwa wanatafuta mawazo mapya katika kipindi cha COVID19 ndio wakaona wazo lao litasaidia mamilioni ya wanafunzi ambao walikuwa majumbani na kuamua kuliwasilisha ambapo waliibuka nafasi ya pili.

“Fedha tulizoshinda katika mashindano ya Youth connekt tulinunulia vifaa, tuna camera, taa, sehemu ya kuwekea vipindi vyote tunavyozalisha na pia kompyuta tunazozitumia katika uzalishaji wa vipindi. “

Vijana hao hawana utaalamu wa kuendesha biashara UNDP imehakikisha wanapata mafunzo hayo pia

“Pia tumepata mafunzo ya kina ya ujasiriamali na tumejifunza kuhusu masoko na kuendesha biashara kwasababu wengi wetu ni wajasiriamali kwa mara ya kwanza kwahiyo tunajifunza sana kadri tunavyoendelea kufanya kazi, madarasa ya kujifunza tunayoshiriki yamekuwa na manufaa sana kwetu.”

Mbali na jukaa hilo la cheza na jifunze au kwa kiingereza Playandlearn wameweza kutumia elimu ya ujasiriamali waliyopata katika kuanzisha biashara ya kupiga picha na video na kujipatia kipato cha Zaida kwakutumia vifaa vilevile walivyonunua kwa fedha walizopatiwa na UNDP.

Kuhusu mashindano ya wajasiriamali chipukizi #YouthConnektZim

Mwaka 2020 katikati ya janga la CORONA shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa maendeleo duniani, UNDP Zimbabwe lilikaribisha vijana kutoka kila pembe ya nchi hiyo kuwasilisha mapendekezo ya bidhaa au huduma ambazo wametengeneza ambazo zinatumika kupunguza na kukomesha kuenea kwa coronavirus.

Takriban maombi 200 yalipokelewa na UNDP kutoka kote nchini yakiwemo biashara mbalimbali zikiwemo programu za COVID19, jumbe zitakazotumwa machine katika mtandao wa Whatsapp, Vifaa vya Kujikinga (PPE), video za uhuishaji zenye taarifa kuhusu COVID19 na majukwaa ya kujifunza kielektroniki.

Maombi yalikaguliwa na jopo la wataalamu wakiwemo wawakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani WHO ili kuhakikisha kuwa bidhaa au huduma zilizochaguliwa zinafaa kwa soko na washindi kumi walitangazwa.

Kufahamu zaidi kuhusu shidano hili bofya hapa