Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwazi wa teknolojia kwenye sayansi utanufaisha dunia nzima: WHO

William G. Dundon, mshauri na mwanabaiyolojia wa molekyuli FAO/IAEA akiandaa kutenganisha dutu za kijenetiki za virusi kwa ajili ya uchunguzi.
IAEA/Dean Calma
William G. Dundon, mshauri na mwanabaiyolojia wa molekyuli FAO/IAEA akiandaa kutenganisha dutu za kijenetiki za virusi kwa ajili ya uchunguzi.

Uwazi wa teknolojia kwenye sayansi utanufaisha dunia nzima: WHO

Afya

Baraza la wataalamu wa Sayansi la Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limetoa ripoti yake ya kwanza likitaka kuwepo na usawa wa kupatikana teknolojia ya kusoma vinasaba au Genomics baina ya nchi tajiri na zile zinazoendelea duniani. 

Ripoti hiyo imehoji na kueleza haikubaliki kimaadili na hata kisayansi kwa nchi zisizo na rasilimali kupata ufikiaji wa teknolojia kama hizo muda mrefu baada ya nchi tajiri kufanya hivyo.

Baraza hilo limeeleza kuwa usambazaji kwa usawa wa teknolojia hizi ni muhimu kwa ajili ya kufikia manufaa makubwa yanayoweza kutokea kwa afya ya binadamu wote.

“Ni dhahiri kwamba teknolojia ya kusoma vinasaba inaweza kutoa mchango mkubwa kwa afya ya binadamu, kuanzia kwenye uchunguzi wa idadi ya watu kama mawakala wa maambukizi kama vile virusi vinavyosababisha coronavirus">COVID-19, kutabiri na kutibu magonjwa mbalimbali kama saratani pamoja na shida za ukuaji” Amesema Mwenyekiti wa Baraza hilo Profesa  Harold Varmus, ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Nobel na Mkurugenzi wa zamani wa Taasisi za Kitaifa za Afya za Marekani.

Picha iliyotengenezwa kidijitali ikionesha maambukizi ya kirusi cha corona katka rangi ya buluu, kisa cha kwanza kilichogundulika Marekani
CDC/Hannah A Bullock/Azaibi Tami
Picha iliyotengenezwa kidijitali ikionesha maambukizi ya kirusi cha corona katka rangi ya buluu, kisa cha kwanza kilichogundulika Marekani

Baraza hilo limeeleza utaalamu wa kutumia teknolojia hiyo ni muhimu sana si kwa binadamu pekee bali hata kwenye kilimo kwakuwa hutumia njia za kibaiolojia na kikemia ili kupata uelewa wa taarifa za kibaiolojia katika vinasaba ambazo zinakuwa na manufaa kwenye utengenezaji wa dawa na pia masuala ya afya kwa umma wakitolea mfano wakati wa janga la COVID-19. 

Mwanasayansi mkuu wa WHO Dkt.Soumya Swaminathan amesema “Teknolojia hizi zinasaidia katika tafiti ambazo ugunduzi wake umekuwa na manufaa makubwa sana, hata hivyo manufaa ya nyezo hizi hazitatumika ipasavyo mpaka hapo zitakapo achiwa zitumike duniani koye. Ni kwa njia ya usawa pekee ndipo sayansi inaweza kufikia matokeo yake kamili na kuboresha afya kwa  kila mtu kila mahali.”

Ripoti hiyo imeeleza nchi kama Afrika kusini wakati wa janga la COVID-19 ilitoa mchango muhimu katika kugundua anuwai mpya kwasababu ya uwezo wao katika eneo hili. 

Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na WHO zinaonesha asilimia ya nchi zinazowezo kufanya uchunguzi wa kutumia utaalamu wa kusoma vinasaba zimeongezaka kutoka 54% hadi 68% kati ya  mwezi machi 2021 na Januari 2022 kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa wakati wa janga la COVID-19.

Pamoja na mambo mengine ripoti hiyo pia imetoa mapendekezo kwenye maeneo kadhaa ikiwemo ushirikiano, masuala ya kijamii, uchechemuzi na masuala mengine ya kimaadili na kisheria. 

Kusoma zaidi kuhusu ripoti hiyo bofya hapa