Dola bilioni 1.5 zahitajika ili kusaidia elimu ya watoto milioni 20 katika migogoro:ECW

20 Septemba 2022

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Elimu haiwezi kusubirti, Education Cannot Wait (ECW) ambao ni mfuko wa kimataifa wa elimu katika maeneo ya dharura na migogoro ya muda mrefu, leo umetoa ombi kwa viongozi wa dunia kutoa dola bilioni 1.5 za ufadhili wa dharura kusaidia mfuko huo wa kimataifa wa umoja wa Mataifa kwa ajili ya elimu na wadau wake.

Mfuko wa ECW unasema nia ya ombi hilo ni kuweza kuwafikia watoto na barubaru milioni 20 walioathirika na migogoro katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Hatua hii mpya ya uwekezaji na mpango makati wake wa mwaka 2023-2026 umeweka dhamira mpya, yenye nguvu na imara  kwa mfuko huo wa ufadhili wa Umoja wa Mataifa, ambao tayari umekusanya zaidi ya dola bilioni moja hadi sasa  na kusaidia moja kwa moja takriban watoto na vijana milioni 7 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016, na wengine milioni 31.2 katika hatua zake za vita dhidi ya janga la COVID-19.

Tathimini ya hivi karibuni kutoka kwa mfuko wa elimu haiwezi kusubiri  inaonyesha kuwa takriban wasichana na wavulana milioni 222 walioathiriwa na migogoro wanahitaji msaada wa haraka wa elimu. 

Na zaidi ya milioni 78 kati ya watoto hawa hawaendi shuleni,huku wengine takriban milioni 120 hawajafikia ujuzi wa chini wa kusoma au hesabu.

Hivyo mfuko huo wa ECW unasema fedha za ombi hilo zitapiga jeki kwa kiasi kikubwa juhudi zake za kuhakikisha watoto na vijana walio katika mazingira magumu wanapata elimu saw ana wengine.

 

  

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter