Chuja:

migogoro

14 FEBRUARI 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia changamoto za usalama mashariki mwa nchi hiyo hususan jimboni Ituri. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo WHO, watoto katika maeneo ya migogoro na haki za raia nchini Zimbabwe. Mashinani tutasalia hapa makao maku ya Umoja wa Mataifa, kulikoni?

Sauti
10'58"
© UNICEF/Ashley Gilbertson VII Photo

Rekodi ya wakimbizi milioni 100 ni rekodi ambayo haikupaswa kuwekwa kamwe-Grandi

Idadi ya watu waliolazimika kukimbia migogoro, ghasia, ukiukwaji wa haki za binadamu na mateso sasa imevuka hatua ya kushangaza ya watu milioni 100 kwa mara ya kwanza kwenye rekodi, iliyochochewa na vita vya Ukraine na migogoro mingine inayosababisha maafa limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR

Sauti
2'58"

31 DESEMBA 2021

Katika jarida la matukio ya mwaka la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Wanajeshi watatu wa kulinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA, wamejeruhiwa na mmoja vibaya sana baada ya msafara wao kukanyaga vilipuzi. Wote wanatibiwa hospitalini mjini Bangui

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema mwaka huu umekuwa wa machungu na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto katika mizozo ya muda mrefu na ile mipya. 

Sauti
12'7"

Juni 25 2021

Katika uchambuzi wa habari zetu hii leo Ijumaa  tutaelekea nchini Afghanistan kutazama namna mradi wa ukarabati wa mfereji wa umwagiliaji ulivyobadilisha maisha ya wananchi. Pia tutajifunza Kiswahili katika Neno la wiki, Dkt. Mwanahija Ali Juma Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar BAKIZA anafafanua maana ya msemo " IMANI YA DAKTARI. 

Sauti
10'19"
UN Women/Allison Joyce

Tunao wajibu wa kutekeleza ahadi ya kutokomeza migogoro-Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake wa siku ya wakimbizi duniani ameeleza ahadi ya Umoja wa Mataifa kukomesha migogoro na mateso yanayosababisha mamilioni ya watu kuwa wakimbizi. Loise Wairimu anaarifu zaidi.

Bwana Guterres amesema kuwa Umoja wa Mataifa unaahidi kufanya kila lililo katika uwezo wake kukomesha migogoro na mateso ambayo imesababisha takribani watu milioni 80 wanawake, watoto na wanaume kote duniani kuyakimbia makazi yao na kujikuta ukimbizini.

Sauti
2'3"