Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zichukuliwe sasa kulinda mazingira la sivyo binadamu watageuka kafara: wataalam UN 

Wanaharakazi vijana wakishiriki mgomo kwa ajili ya kuchagiza kuhusu mabadiliko ya tabianchi Stockholm, Sweden.
© UNICEF/Christian Åslund
Wanaharakazi vijana wakishiriki mgomo kwa ajili ya kuchagiza kuhusu mabadiliko ya tabianchi Stockholm, Sweden.

Hatua zichukuliwe sasa kulinda mazingira la sivyo binadamu watageuka kafara: wataalam UN 

Haki za binadamu

Miongo mitano baada ya kongamano la kwanza la dunia la kufanya mazingira kuwa suala kuu, wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wametoa wito kwa mataifa kuongeza juhudi za kulinda sayari iliyo hatarini kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo huku kukiwa na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa za mazingira na nyinginezo.

Baadhi ya jamii zinateseka kutokana na ukosefu wa haki za kimazingira ambako uchafuzi wa mazingira na vitu vyenye sumu ni mkubwa sana mpaka maeneo hayo yamnelezwa kuwa “maeneo ya kafara,” wamesema wataalam hao.  

Wameongeza kuwa "Kwa kuzingatia mwelekeo wa wanadamu kuhusu vitu vyenye  sumu, mabadiliko ya tabianchi, na upotezaji wa bayoanuai, sayari iko katika hatari ya kuwa eneo la kafara ya wanadamu." 

David Boyd,  maalumu maalum wa haki za binadamu na mazingira, ameyataka Mataifa kuweka haki ya mazingira yenye afya katikati ya majadiliano na matokeo yote katika mkutano wa Stockholm+50 utakaofanyika tarehe 2 na 3 Juni, na kutekeleza mabadiliko ya katiba na sheria za mazingira, zinazotokana na utambuzi wa haki ya mazingira yenye afya. 

Naye Marcos Orellana, mtalaam wa Umoja wa Mataifa kuhusu taka za sumu na haki za binadamu  amreutaka mkutano wa Stockholm+50 jinsi gani haki za binadamu zilivyochagiza vipengele muhimu vya azimio la mwaka 1972  la Stockholm.  

"Huu ni wakati muhimu kwa sheria ya kimataifa ya mazingira kubadili mwelekeo na kukumbatia mkabala wa haki za binadamu wa ulinzi wa mazingira," amesisitioza.” 

Uchafuzi wa plastiki unadhuru mazingira nchini Haiti.
IOM
Uchafuzi wa plastiki unadhuru mazingira nchini Haiti.

Miaka 50 ya azimio la Stockholm 

Dhana ya haki ya mazingira yenye afya inatokana na azimio la Stockholm la mwaka 1972. "Leo, miaka 50 baadaye, mkutano wa Stockholm+50 unawakilisha jukwaa bora la kukaribisha kwa shauku utambuzi wa hivi karibuni wa Umoja wa Mataifa wa haki hii wakati pia kubainisha hatua za haraka zinazohitajika kwa utekelezaji wake," wamesema wataalam hao. 

"Kuweka haki za binadamu katikati ya hatua za kimazingira kutakuwa na athari chanya kwa ubora wa hewa, maji safi, udongo wenye afya, chakula kinachozalishwa kwa uendelevu, nishati ya jadidifu, mabadiliko ya tabianchi, bayoanuwai na uondoaji wa taka za sumu na ulinzi wa haki za watu wa asili. Kufanya hivyo kuna uwezekano wa kuleta mabadiliko na kuokoa Maisha ya mamilioni ya watu kila mwaka.” 

Tarehe ya kukumbuka 

Mwezi Oktoba 2021, katika azimio la kihistoria, Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva lilitambua kwa mara ya kwanza haki ya binadamu ya mazingira safi, yenye afya na endelevu. 

Azimio hilo liliashiria kilele cha juhudi za miongo kadhaa za mashirika ya kiraia, yakiwemo makundi ya vijana, taasisi za kitaifa za haki za binadamu na watu wa asili. 

Familia za wakimbizi zikihaha kusaka maji katika mazingira ya baridi kali kwenye mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.
© UNHCR/Andrew McConnell
Familia za wakimbizi zikihaha kusaka maji katika mazingira ya baridi kali kwenye mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Kaye na Orellana, pamoja na wataalam huru wenzake maalum Francisco Calí Tzay na Ian Fry, walichagiza mataifa kulihimiza Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuzingatia na kutambua haki ya mazingira safi, yenye afya na endelevu kwa urahisi wake, kama vile Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lilivyofanya. 

Wito wa Baraza Kuu 

"Azimio la Baraza Kuu juu ya haki ya mazingira yenye afya litaimarisha uharaka wa hatua za kutekeleza haki," wamesema katika taarifa, na kuongeza kuwa "Sote tuna bahati ya ajabu kuishi katika sayari hii ya ajabu, na lazima tutumie haki ya mazingira mazuri ili kuhakikisha serikali, biashara na watu wanafanya kazi bora zaidi ya kutunza nyumba ambayo sisi sote tunashiriki." 

Wataalam hao maalum na huru huteuliwa na Baraza la Haki za Kibinadamu kuchunguza na kutoa ripoti kuhusu mada maalum ya haki za binadamu au hali ya nchi. Wako huru kutoka kwa serikali yoyote na hawalipwi kwa kazi yao.