Hatimaye Kenya imeibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya ujumbe usio wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya kuishinda Djibouti.
Ijapokuwa yaonekana kuwa dunia nzima iko kwenye karantini ikiwa ni masharti ya kiafya ili kuepuka kusambaza virusi vya ugonjwa wa Corona au COVID-19, vikao vya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya chombo hicho chenye wanachama 193 vinaendelea, kwa kutumia teknolojia.
Akitoa taarifa ya kufunga mjadala Mkuu wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York hii leo Rais wa Baraza Kuu Tijjani Muhammad-Bande amesema ushirikiano wa kimataifa unasalia kuwa nguzo muhimu inayokubalika na kutegemewa katika kutatua changamoto za kimataifa miongoni mwa nchi wanachama.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limechagua nchi tano wanachama wa umoja huo ambao watachukua ujumbe usio wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuanzia mwezi Januari mwakani.
Mkutano wa 72 wa Baraza la shirika la afya duniani, WHO umeanza leo mjini Geneva, Uswisi ukilenga kutathmini mwelekeo wa afya duniani na harakati za kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan yale yahusuyo afya.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena wamepitisha kwa kishindo azimio linalosisitiza umuhimu wa kumaliza vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba.