Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa kimataifa unasalia kuwa nguzo ya suluhu ya kimataifa-Muhammad

Tijjani Muhammad-Bande(Kuahoto) Rais wa mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifaafunga mjadala wa wazi Septemba 30, 2019.
UN Photo/Cia Pak
Tijjani Muhammad-Bande(Kuahoto) Rais wa mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifaafunga mjadala wa wazi Septemba 30, 2019.

Ushirikiano wa kimataifa unasalia kuwa nguzo ya suluhu ya kimataifa-Muhammad

Masuala ya UM

Akitoa taarifa ya kufunga mjadala Mkuu wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York hii leo Rais wa Baraza Kuu Tijjani Muhammad-Bande amesema ushirikiano wa kimataifa unasalia kuwa nguzo muhimu inayokubalika na kutegemewa katika kutatua changamoto za kimataifa miongoni mwa nchi wanachama.

Amewashukuru washiriki wote katika mjadala huo wa ngazi ya juu hali kadhalika mikutano mingine mbalimbali kandoni mwa mjadala mkuu ambayo imedhihirisha nguvu ya ushirikiano wa kimataifa.”Ni matumaini yangu kwamba ari na hamasa iliyoonekana wakati wa mjadala mkuu itadhihiroisha thamani yake wakati huu tukielekea maadhimisho ya 75 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa na wakati huu tukiungana pamoja kushughulikia changamoto za sasa zinzoikabili dunia.”

Ameongeza kuwa pamoja na kwamba kuna maswali yanayozuka kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa, na hata wakati ambao hatukubaliani jinsi gani dunia iendeshwe au kuratajia jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazoongezeka duniani , hatimaye ni lazima tufikie muafaka wa pamoja kuhusu haja ya kuwa na utulivu wa kimataifa kwa kuzingatia misingi ya sheria.

Amesisitiza kuwa “Katika duniani hii iliyoghubikwa na kudumazwa na changamoto nyingi , ushirikiano wa kimataifa ndio njia pekee ya kuhakikisha amani, usalama, na maendeleo endelevu. Dunia hii haiwezi kudumu kwa kmuda mrefu isipokuwa tu kwa dhamira ya kutoa na kupokea ambayo ndio kiini cha ushirikiano wa kimataifa”

Amesema hata waleo ambao bado wana shuku kuhusu hilo ushiriki wa nchi wanachama 192 katika ya 193 kwa mjadala wa mwaka huu ni ishara dhahiri ya kutambua ushirikiano na kutegemeana miongoni mwa mataifa

Hafla ya kufunga mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na rais wa Baraza Kuu Tijjani Muhammad-Bande. Septemba 30, 2019
UN Photo/Cia Pak
Hafla ya kufunga mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na rais wa Baraza Kuu Tijjani Muhammad-Bande. Septemba 30, 2019

Ushiriki wa viongozi wanawake

Akigeukia suala la usawa wa kijinsia katika mjadala huo wa ngazi ya juu Rasia wa Baraza Kuu Tijjani Muhammad-Bande amesema “Baraza kuu ni miongoni mwa vyombo vyenye uwakilishi mkubwa katika Umoja wa Mataifa hata hivyo inaumiza kuona kwamba wiki hii wanawake 16 pekee kati ya wazungumzaji 192 ndio walikuwa wanawake, hivyo napozungumzia uwakilishi katika Umoja wa Mataifa kwa hakika hatumaanishi hali hii.”

Kwa kusema Umoja wa Mataifa jumuishi tunamaanisha chombo ambacho kitamruhusu kila binadamu kufikia ukomo wa uwezo wake, bila kuzuiliwa kwa misingi ya jinsia au historia ya kutojiweza. Usawa wa kijinsia katika ulimwengu wa sasa bado ni mchakato.

Hivyo tunahitaji kuongeza mara mbili juhudi zetu kuchapuza mchakato huo ikiwemo sio tu kuongeza wanawake katika ngazi ya maamuzi bali pia katika orodha ya wazungumzaji wanaotakiwa kuwakisha katika mikutano ya ngazi ya kimataifa. Natoa wito kwa kila mmoja wetu kutoa nafasi kwa wanawake , na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika ngazi zote za kufanya maamuzi.

Mchango wa vijana

Wiki ya mkutano wa ngazi ya juu vijana walidhihirisha dhamira yao walipoaandamana kwa mamilioni kote duniani  na kimsingi kuchukua hatamu za Baraza Kuu wakati wa mkutano wa ngazi ya juu wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.”  Vijana ngoja niwahakikishie, tumewasikia , lakini kuwasikia tu haimaanishi mpunguze sauti. Endeleeni kupaza sauti zenu msikike zaidi kila wakati mpatapo fursa. Mada mbalimbali zilitamalaki kwenye wiki ya madala wa ngazi ya juu kuanzia hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi  na pia kupitishwa kwa azimio la kisiasa la kihistoria kuhusu huduma za afya kwa wote zikijikita na kuzuia, kuchagiza na kufikisha huduma bora za afya. Haya ni mafanikio makubwa amesema Rais wa Baraza Kuu. Vivyo hivyo ameongeza kuwa “Mkutano wa malengo ya maendeleo endelevu SDGS ulimalizika kwa kupitishwa azimio la kisiasa lililobeba kichwa “Mchakato kwa ajili ya muongo wa hatua na ufikiaji wa malengo ya maendeleo endelevu.” Kazi yetu inaongozwa na ajenda ya 2030 amesema lakini ilibidi pia kutafakari miaka 30 iliyopita tangu kupitishwa mkartaba wa haki za mtoto na sherehe maalum itafanyika mwezi Novemba.

Miaka 75 ya UN

Rais wa Baraza Kuu amegusia pia kuwa ni takribani miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuihakikishia dunia amani na usalama.

Wiki hii ya mkutano wa ngazi ya juu tumeshuhudia mafanikio mengine katika kusongesha aman imbele ikiwemo maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza silaha za nyuklia na pia kutiwa saini na kuridhia mkataba wa kupinga silaha za nyuklia.

Matukio haya ni kutokana na juhudi za nchi wanachama katika kuelekea kuwa na dunia huru bila silaha za nyuklia.

Mikutano mingine muhimu

Pia kumekuwa na mkutano wa kwanza kabisa wa ngazi ya juu kwa ajili ya ufadhili wa maendeleo tangu kupitishwa kwa mkataba wa Addis Ababa ambao umechagiza kukusanya fedha za ziada zinazohitajika takribani dola trilioni 2.4.

Na mkutano wa mwisho wa ngazi ya Rais wa Baraza Kuu amesema ni kutatjimini mchakato wa visiwa vidogo vinavyoendelea (SIDS) kupitia mchakato wa SAMOA.

Amesema bila shaka mataifa hayo yamedhihirisha mnepo wa hali ya ju una uongozi bora katika wakati mgumu, na sasa ni jukumu kwa dunia kuzisaidia nchi hizo kwa kila njia inayowezekana na kuhakikisha kwamba wanashirikia kama washirika wenye hadhi sawa katika uchumi wa kimataifa , “ kwa kuzisaidia nchi hizo za visiwa vidogo tunajisaidia wenyewe na kusihi kwa kutekeleza misingi inayohitajika ya ubinadamu wetu.”

Amesema viongozi wengi wa dunia wamezungumzia changamoto zinazofanana kama vita, ghasia za itikadi Kali, uzalishaji wa nyuklia , wahamiaji, mabadiliko ya tabianchi na kuendelea kwa pengo la usawa.

Na hivyo amesisitiza kwamba baada ya kuzitaja changamoto hizo sasa ni lazima kuschukua hatua za kusonga mbele kwa pamoja kuzicshughulikia katika mwaka mzima wa kikao cha 74 cha UNGA.