Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO kupitia mradi wake wa FISH4ACP walenga kuwawezesha wanawake katika biashara ya uvuvi,Tanzania

Mradi wa FISH4ACP wa kuongeza mnyororo wa thamani katika sekta ya uvuvi umepelekwa pia mkoani Katavi kusini-magharibi mwa Tanzania.
UN Tanzania
Mradi wa FISH4ACP wa kuongeza mnyororo wa thamani katika sekta ya uvuvi umepelekwa pia mkoani Katavi kusini-magharibi mwa Tanzania.

FAO kupitia mradi wake wa FISH4ACP walenga kuwawezesha wanawake katika biashara ya uvuvi,Tanzania

Ukuaji wa Kiuchumi

Shirika la Umoja wa Mataifa la  Chakula na Kilimo FAO kupitia mradi wake wa FISH4ACP limefanya mkutano wa pili wa Kikosi Kazi cha Taifa cha kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma lengo likiwa ni kuimarisha na kujenga mazingira rafiki kwa wanawake ili kufanya shughuli zao katika nyanja ya uchakataji, wafanyabiashara na usafirishaji na kuongeza kipato binafsi na pato la Taifa.

Hashim Muumin ni Afisa Mtaalamu Mnyororo wa Thamani wa Uvivu na Ufugaji Viumbe Maji, kutoka FAO nchini Tanzania anayesimamia mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma nchini Tanzania amesema utafiti unaonesha kwamba kuna changaoto kwa wanawake wavuvi ambao ni asilimia 87 ya wafanyabiashara wa uvuvi wa wa ziwa Tanganyika hususan wachakataji na kwa akutambua changamoto hizo watazifanyia kazi ili kuzitatua.


Afisa Mtaalamu huyo amesema watazingatia usimamizi wa biashara za wanawake na uongozi kwa kutafuta mbinu za kuwawezesha kuongoza vikundi vyao na wapatiwe fursa ya kuchangia katika sekta ya uvuvi ya ziwa Tanganyika.