Zambia: FISH4ACP kusaidia uvuvi endelevu wa dagaa Kapenta na samaki buka
Nchini Zambia, wafanyabiashara ya samaki kandokando ya Ziwa Tanganyika wameanza kuwa na wasiwasi kuwa uvuvi usizingatia kanuni za uvuvi bora unaweza kuhatarisha ustawi wao ambao unategemea biashara ya dagaa aina wafahamikao nchini humo kama Kapenta na samaki aina ya Buka.