Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wavuvi ziwa Tanganyika nchini Tanzania wazindua kikosi kazi cha kusimamia mnyororo wa thamani

Wajumbe wa bodi ya mnyororo wa thamani wa uvuvi  ziwa Tanganyika nchini Tanzania
UN News
Wajumbe wa bodi ya mnyororo wa thamani wa uvuvi ziwa Tanganyika nchini Tanzania

Wavuvi ziwa Tanganyika nchini Tanzania wazindua kikosi kazi cha kusimamia mnyororo wa thamani

Ukuaji wa Kiuchumi

Mradi wa FISH4ACP unaotekelezwa katika mikoa mitatu ya Kigoma, Rukwa na Katavi nchini Tanzania chini Shirika la Chakula na Kilimo FAO umezindua Kikosi Kazi cha Kitaifa  chenye wajumbe 16 cha kusimamia  mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi ziwa Tanganyika.

Uvuvi ni moja ya sekta ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa mtu mmoja mmoja na kupambana na umasikini hata kuchangia pato la Taifa.

Kufuatia hilo Mradi wa FISH4ACP unaotekelezwa katika mikoa mitatu ya Kigoma, Rukwa na Katavi nchini Tanzania chini Shirika la Chakula na Kilimo FAO umezindua Kikosi Kazi cha Kitaifa  chenye wajumbe 16 cha kusimamia  Mnyororo wa Thamani wa mazao ya uvuvi Ziwa Tanganyika.

Betina Tito ambaye ni mchakataji katika Mwalo wa Kibirizi mkoani Kigoma analipongeza Shirika hilo kwa kuanzisha mradi utakaosaidia kuongeza myororo wa thamani ya mazao ya uvuvi.

“Mradi ni mzuri inatupa jinsi gani mnyororo ule wa thamani yaani mpaka samaki atakapofika hatua ya mwisho iwe kwa msafirishaji au mlaji atafika akiwa na viwango bora hii hatua ya kuundwa  kikosi kazi itarahisisha kwa sababu itatutoa tulipokuwa kwenye zana za zamani na kutuleta kwenye zana nzuri na itaturahisishia maisha na kujua nini tufanye ili tunufaike na uchakataji wetu,”Amesema Betina.

Mwingine  aliyefanikiwa kuhudhuria kikao hicho  ni Francis John ambaye ni Mwenyekiti wa Vyama vya Ushirika wa Wavuvi Mkoa wa Kigoma anaeleza hali ya uvuvi ilivyokuwa awali kabla ya mradi huo.

“Kigoma tutapata fursa kazi zitapatikana leo tulikuwa tunashindwa kusafirisha samaki hazipo kulingana na vyombo ni vichache Samaki migebuka maana Marekani wanapenda migebuka na dagaa lakini tunaamini mialo ikisafishwa , ikataengenezwa  tukapata sehemu nzuri ya kuchakatia Nchi yetu yenyewe itapata mapato mazuri na wafanyabiashara tutapata faida kwa sababu tutasafirisha dagaa na Samaki kupeleka Canada, Austrelia, Marekani na kwingineko,” Ameleeza Francis.

Wavuvi Kigoma Tanzania
UN News
Wavuvi Kigoma Tanzania

Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, Abdul Balozi akawataka wavuvi, wachakataji na wasafirishaji kuzingatia sheria ili kufanya shughuli zao katika mazingira salama.

“Wito wangu kwa wavuvi na wadau wote wanaojihusisha na masuala ya uvuvi kwanza ni kuzingatia sheria pia kufuata mbinu bora za uchakataji, uvuvi na ufanyaji biashara bora kukidhi matakwa ya biashara zao kwa ujumla kwa kufanya hivyo ndiyo tutafikia lengo la kunyanyua mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi kuanzia kwa mvuvi hadi  kwa mlaji,”Amebainisha Abdul.

Sikuishia hapo nilikutana na Mteknolojia Mwandamizi Chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Afisa Dawati wa Mradi wa FISH4ACP, Masui Munda anatuambia majukumu ya kikosi kazi.

“Jukumu kuu na la jumla ni hilo kusimamia shughuli za mradi lakini majukumu mengine sasa ni kikosi kazi hiki kujigawa katika maeneo mahususi ya mradi kuona namna gani vikundi vidogo vidogo vitasimamia kazi za utendaji katika meneo hsika ukingatia kwamba mradi una maeneo manne kwanza kuongeza thamani kwa kutumia teknolojia iliyoboreshwa katika kuchakata na kuhifadhi mazao ya uvuvi, kuwawezesha kina mama katika mnyororo wa thamani, kuja na model ya biashara na lingine lile linalohusika na sheria za uvuvi na sheria zingine,” Amesema Masui.

Na Hashim Muumin ni Mratibu wa mradi wa FISH4ACP kutoka FAO anabainisha maeneo yatakayozingatiwa wakati wa utekelezaji wa mradi.

“ Eneo la kwanza ni kuimarisha uchakataji wa dagaa na samaki aina ya migebuka inayotoka Ziwa Tanganyika, kuboresha mifumo ya barafu ambayo wanatumia wavuvi na wanaonunua Samaki katika mialo yao na kupeleka maeneo wanayochakata, eneo lingine kuimarisha hivi vikundi vya  BMU vikundi vya kijamii vya usimamizi wa uvuvi tunategemea kwamba hata uchumi wa wavuvi na wadau wa uvuvi wa Ziwa Tanganyika utaimarika,” Amefafanua Hashim.