Usawa wa jinsia kwenye uvuvi kunasua wanawake kiuchumi
Malengo ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, au SDGs yanafikia ukomo mwaka 2030 ikimaanisha imesalia miaka 7 kufikia ukomo. Sasa Umoja wa Mataifa unachagiza utekelezaji wa malengo hayo ikiwemo lile la kutokomeza umaskini na usawa wa kijinsia kama nija mojawapo ya kuinua kaya kiuchumi.