Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Soka

Global Youth Forum/Peter Omondi

Vijana Kenya watumia mpira wa miguu kutokomeza umasikini na kuishi maisha bora - Peter Omondi

Katika kuelekea siku ya kandanda, kabumbu au mpira wa miguu duniani itakayoadhimishwa Jumapili wiki hii Mei 25 ikibeba maudhui nguvu ya kdandanda katika kuleta mabadiliko tuabisha hodi Nairobi Kenya ambapo leo Peter Omondi, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Global Youth Forum linalounganisha vijana Kenya kwa lengo la kutokomeza umasikini na kuishi maisha bora kupitia michezo mbalimbali ikiwemo kandanda akizungumza na Idhaa hii ya Kiswahili anaeleza umuhimu wa kandanda katika ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu. Anaanza kwa kujitambusha.

Sauti
3'6"

23 MEI 2025

Hii leo jaridani tunaangazia haki za kibinadamu za raia nchini Uganda, na simulizi ya mkimbizi nchini Mexico ambaye alikimbia machafuko nchini mwake Haiti. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Ethiopia, kulikoni?

Sauti
9'56"
UN News/Ziad Taleb

Mohamed hajakata tamaa ya kuwa mwanasoka maarufu - Gaza

Katika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo. 

Sauti
1'53"
Mohamed Abu Jalda, anachezea Klabu ya Soka ya huduma za Rafah.
UN News/Ziad Taleb

Gaza: Mohamed hajakata tamaa ya kuwa mwanasoka maarufu

Katika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo.

Sauti
1'53"

26 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo alihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa na kutangaza kuwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwishoni mwa mwaka huu, utafanyika kama ilivyopangwa. Alisema tayari Tume Huru ya Uchaguzi nchini DRC, CENI [SENI] imeshachapisha majina ya wagombea na michakato mingine inaendelea.

Sauti
11'49"
UN News

Mradi wa "Football for the Goals" kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu Rwanda - UN Rwanda

Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia chepuo mbinu mbali mbali halali za kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs, na miongoni mwa mbinu hizo ni mpira wa miguu, soka, wengine wakisema kabumbu au kandanda! Sasa wenyewe wabobezi au manguli wa soka wameitikia wito na Umoja wa Mataifa hususan nchini Rwanda ukaitikia Naam!!! Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ameketi na Mkuu wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa UN, Rwanda Josephine Marealle-Ulimwengu na anafafanua kitendawili hicho.

Sauti
6'43"

01 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunaangazia mabadiliko ya tabianchi na malelengo ya maendeleo endelevu kupitia mchezo wa mpira wa miguu. Makala tutaelekea nchini DRC kusikia simulizi ya wakimbizi na mashinani tunakupeleka nchini Tanzania kusikia ni kwa vipi wanawake wameweza kufanya kazi zao na kunyonyesha watoto wao ipasavyo.

Sauti
12'14"
OSCE

Global Youth Forum  na UNIS Nairobi watekeleza mradi wa ‘Football for the Goals’ kwa vitendo

Mwaka jana 2022 mwezi Julai, katika siku ya kwanza ya Michuano ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Barani Ulaya chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani humo (UEFA Women's EURO 2022), Umoja wa Mataifa uliitumia siku hiyo kuzindua mradi wa ‘Football for the Goals’ yaani Mpira wa Miguu kwa ajili ya Malengo ukiwa ni mpango mpya wa Umoja wa Mataifa ambao unatoa jukwaa kwa jumuiya ya soka duniani kujihusisha na kuhamasisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Nchi ziliitikia na mradi huo unaendelea duniani kote.  

Sauti
2'41"

26 JULAI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNESCO kuhusu teknolojia na pia afya ya wanawake wajawazito nchini Sudan. Makala tunakupeleka nchini Australia na mashinani Roma nchini Italia, kulikoni? 

Sauti
13'7"