Michezo ni faraja ya mwili na akili kwa vijana:UNMISS

Picha: UNMISS
Wachezaji wa timu ya taifa ya soka Sudan Kusini, Bright Star katika mazoezi na kocha wao kutoka Korea Kusini kabla ya kuondoka kwenye Msumbiji.

Michezo ni faraja ya mwili na akili kwa vijana:UNMISS

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Vita vinavyoendelea Sudan Kusini vimesababisha madhara makubwa  ikiwemo msongo wa mawazo miongoni mwa vijana lakini pia vimekatili maisha ya maelfu na mamilioni kuwafanya wakimbizi wa ndani na nje. Sasa michezo inatumika kama tiba ya akili hususan kwa vijana. 

Malakal Sudan kusini vijana wakiwa uwanjani wanasakata kabumbu, kwao ikiwa ni moja ya fursa za kufahi na wenzao, lakini pia kupunguza msongo wa mawazo walionao kwa kuishi katika nchi ambayo ina fursa finyu sana kwa mustakhbali wao kutokana na vita vinavyoendelea.

Mayom Chol ni mchezaji wa timu ya soka ya Malakali anasema michezo

 

(SAUTI YA MAYOM CHOL)

“Itatusaidia sana katika nyanja nyingi na hasa katika kudhibiti msongo wa mawazo, Kama utakuja kwenye kandanda angalau utatumia muda mwingi kuwa na furaha ukilinganisha na kuwa mpekwe. Na kuanzia hapo hatutakuwa na tatizo lolote.”

Hivi sasa wahandisi wa Uingereza na India wanaohudumu katika mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini UNMISS, wanatumia utaalamu wao kukarabati viwanja vya soka, vya mpira wa wavu na mpira wa kikapu kwenye uwanja wa michezo wa Malakal ili kuwapa fursa vijana wengi zaidi kushiriki michezo. Mhandisi wa UNAMIS kutoka Uingereza, Luteni Nick Lytollis anaongeza

(SAUTI YA NICK LYTOLLIS)

“Nadhani michezo katika nchi yoyote inachangia hali bora. Ni njia nzuri kwa watoto kupoteza wakati, kuwa wakakamavu, ni njia nzuri ya kujenga ari ya pamoja na zaidi ya yote wanafurahia, kitu ambacho nadhani ni cha muhimu kwa mtoto yeyote katika nchi yoyote duniani.”