Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wa Somalia wakutana kujadiliana kuhusu ushiriki wao kuiendeleza nchi yao 

Watoto pamoja na vijana wengine wakicheza katika ufukwe wa Lido mjini Mogadishu
UN Photo/Tobin Jones)
Watoto pamoja na vijana wengine wakicheza katika ufukwe wa Lido mjini Mogadishu

Vijana wa Somalia wakutana kujadiliana kuhusu ushiriki wao kuiendeleza nchi yao 

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Vijana wa Somalia wametakiwa kuwa waleta mabadiliko na kushiriki kikamilifu katika siasa, upatanishi, kuleta amani, uchaguzi na juhudi zinazoendelea za kusaidia kuendeleza nchi yao.

Huu ulikuwa ujumbe mkuu katika mjadala uliowaleta pamoja zaidi ya vijana 30 wanaowakilisha sehemu tofautitofauti za za jamii ya Somali kama vile koo mbalimbali, wanafuzi na hata wale ambao tayari wako katika shughuli mbalimbali.  

Tukio hili lilofanyika mjini Moghadishu limeandaliwa na SYCO ambalo ni shirika la vijana lisilo la kiserikali nchini Somalia wakisaidiwa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNSOM. Abdiwaasa Idriss Jelle ni Mkurugenzi wa shirika la vijana wa Somali anasema,“nchi inaokolewa na vijana wake. Ni vijana ambao wanaongoza katika juhudi zote kuleta mabadiliko kwa hivyo ni vizuri kwa vijana pia kushiriki katika sis ana kuwa sehemu ya mabadiliko chanya na maendeleo katika nchi. 

Wanajopo katika hafla hiyo wanabainisha kuwa vijana nchini Somalia wanaunda karibu asilimia 70 ya idadi ya watu wote, na kwa jumla wamewasihi watumie nguvu zao za wingi wa idadi kuhamasisha amani na maendeleo - na jukumu la wanawake vijana likiangaziwa. Bilan Mahamud ni mwanaharakati kutoka Shirika la kitaifa la wanawake wa Somalia anasema, “kwa kuwa wanawake na vijana ni watengeneza historia katika Somalia na wana jukumu katika ujenzi wa taifa, tunawataka kusonga mbele kwasababu tunawataka kutafuta suluhisho la changamoto kubwa tunazokabiliana nazo kama taifa. Vijana hawapaswi kurudi nyuma badala yake wanatakiwa kujitokeza na kuendeleza nchi yao.”  

Baadhi ya washiriki wanasema kwa kushiriki kwao katika majadiliano haya kumewsaidia kuwahamasisha kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa wabunge na pia kushiriki zaidi katika masuala ya kijamii. Mshiriki Fatuma Abdullahi Mahamud anasema, "nimejifunza umuhimu wa vijana katika ujenzi wa amani na sasa nimehamasika kushiriki katika siasa na ujenzi wa amani. Pia nimetambua thamani niliyonayo kama kijana kwa jamii.”