Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana chakarikeni kulinusuru taifa lenu Somalia:Lowcock

Vijana Somalia wamo tayari kushirikiana na serikali ili kukabiliana na ukatili wa kijinsia. Picha: AMISOM

Vijana chakarikeni kulinusuru taifa lenu Somalia:Lowcock

Ukuaji wa Kiuchumi

Vijana nchini Somalia wameelezwa kuwa hakuna taifa duniani linalopenda daima kuwa tegemezi kwa misaada ya dharura. 

Mratibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, Mark Lowcock amesema hayo huko Mogadishu, Somalia wakati akizindua mpango uliopewa jina la "changamoto bunifu kwa vijana".

Amesema ndoto yake itatimia tu endapo wasomali watawezeshwa na kuweza kujimudu

(SAUTI YA MARK LOWCOCK)

"Njia moja tu ya kuona nikitimiza ndoto yangu ya kutohitajika tena kama mratibu wa misaada ya dharura ni kuona mkuu wa UNDP Achim Steiner anafanikiwa kuwasaidia wote. Jinsi ninavyoziona hali nyinyi hilo ndio suluhisho na nawatakia mafanikio mema".

Mpango huo una lengo la kupata mawazo kutoka kwa vijana wakisomali wa jinsi ya kuboresha maisha ya kawaida ya wale waliopoteza makazi yao yaani wakimbizi wa ndani.

Mkuum wa UNDP Achim Steiner amewashauri vijana kuendeleza mitandao ya kimaendeleo ili kukuza ubunifu wao.

(SAUTI YA ACHIM STEINER)

"Tunasaida sana mambo ya dharura, lakini kile tunachopenda sana ni kufanya kazi na wananchi kama nyinyi kwa sababu ikiwa tutawawezesha kufanikiwa na kupiga hatua, nyinyi mtaipeleka somalia mbele zaidi".

Vijana walioshiriki waliwaelezea maafisa wa Umoja wa Mataifa kuhusu fikra zao za kimaendeleo zikiwemo vifaa  mbalimbali vya kutumia katika mitandao, na mbinu bora za kulisha mifugo pamoja na kutengeneza maziwa.