Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yatoa fedha ya dharura dola milioni 40 kusaidia nchi ya Ethiopia

Mtoto mdogo anachunguzwa ukosefu wa lishe bora katika eneo la usambazaji wa chakula huko Tigray, kaskazini mwa Ethiopia.
© WFP/Claire Nevill
Mtoto mdogo anachunguzwa ukosefu wa lishe bora katika eneo la usambazaji wa chakula huko Tigray, kaskazini mwa Ethiopia.

UN yatoa fedha ya dharura dola milioni 40 kusaidia nchi ya Ethiopia

Msaada wa Kibinadamu

Umoja wa Mataifa umetenga dola milioni 40 kutoka kwenye mfuko wake kwa dharura kwa ajili ya kutoa msaada wakibinadamu nchini Ethiopia.

Mratibu Mkuu wa masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa wa Martin Griffiths ambaye amerejea hivi karibuni kutoka nchini Ethiopia amesema “mamilioni ya watu walioko kaskazini mwa Ethiopia wanaishi katika hali duni kutokaa na mzozo unaoendelea, na kueleza kuwa kitendo cha kuongeza fedha hizo kitasaidia mashirika ya misaada kukidhi mahitaji ya watu walio hatarini zaidi ili waweze kulindwa na kupata unafuu wa maisha.”

Griffiths amesema katika maeneo ya Tigray, Amhara na Afar, mgao huo utasaidia mashirika ya misaada kutoa ulinzi na usaidizi mwingine wa kuokoa maisha kwa watu walioathiriwa na mzozo. Wanawake, wavulana na wasichana wanaendelea kubeba mzigo mkubwa wa vita, lakini mahitaji yao ya ulinzi yanabakia kutofadhiliwa.

Msaada wa chakula ukishushwa kutoka kwenye Lori la WFP la kusambaza msaada katika eneo la Zelazle Kaskazini mwa Tigray
© WFP/Claire Nevill
Msaada wa chakula ukishushwa kutoka kwenye Lori la WFP la kusambaza msaada katika eneo la Zelazle Kaskazini mwa Tigray

OCHA inasema katika mikoa iliyoathiriwa na ukame ya Somali na Oromia, ufadhili wa ziada utasaidia kuchukuahatua za haraka kukabiliana na kakabiliana na hali hiyo “mashirika ya kutoa misaada yatatoa maji ya kunywa, ikiwa ni pamoja na kuzuia magonjwa yatokanayo na maji na kupunguza hatari ya kuzuka kwa kipindupindu. Mashirika pia yatasaidia jamii za wafugaji kulinda mifugo yao.”

Msaada huo wa dharura uliotolewa leo kwa Ethiopia umefanya nchi hiyo kwa mwaka huu pekee kupokea jumla ya dola milioni 65, na kuifanya nchi iyo kuwa ya pili iliyopokea msaada mkubwa wa dharura katika mwaka 2021. 

Usaidizi kutoka kwa nchi ya Ethiopia jumla umefikia dola milioni 80 hata hivyo kutokana na hali iliyoko nchini humo jumla ya fedha za ufadhili wanazohitaji ni dola bilioni 1.3 fedha hizi ikiwa ni pamoja na dola milioni 350 kwa ajili ya kusaidia Tigray.