Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna jamii itakayokuwa huru na haki bila waandishi wa Habari:Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani
UN News
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani

Hakuna jamii itakayokuwa huru na haki bila waandishi wa Habari:Guterres 

Haki za binadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza waandishi wa Habari Maria Ressa na Demirty Muratov kwa kushinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu akisema “Duniani kote uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kwa ajili ya amani, haki, maendeleo endelevu na haki za binadamu na ni ngumo muhimu kwa ajili ya ujenzi wa taasisi zenye haki na zisizo na upendeleo.” 

Kupitia taarifa yake ya pongezi kwa washindi hao Guterres amesisitiza kwamba “Hakuna jamii inayoweza kuwa huru na haki bila waandishi wa Habari ambao wanawreza kuchunguza maovu, kufikisha taarifa kwa umma, kuwawajibisha viongozi na kuzungumza ukweli kwa mamlaka.” 

Ameongeza kuwa licha ya ukweli huo bado vyombo vya Habari vinaendelea kupingwa na mashambulizi dhidi ya wanahabari yanaendelea kuongezeka.  

“Tunashuhudia machafuko yakiongezeka na unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari wa ana kwa ana au mtandaoni. Wanawake waandishi wa Habari mara nyingi ndio hususan walengwa wa ukatili huo.” 

Katibu Mkuu amesema wakati huohuo huku teknolojia imebadili njia za watu kupokea na kubadilishana taarifa , pia inatumika kupotosha maoni ya umma au kuchochea machafuko na chuki. 

Uongo  wa kupiga ukweli, na hii haviwezi kuwa kawaida mpya. Uandishi wa habari huru na wa kujitegemea ni mshirika wetu mkubwa katika kupambana na habari potofu na upotoshaji. 

 Tunapowapongeza washindi wa tuzo hii, wacha tuhakikishe tena haki ya uhuru wa vyombo vya habari, tutambue jukumu la msingi la waandishi wa habari na tuimarishe juhudi katika kila ngazi kusaidia vyombo vya habari huru,vya kujitegemea na vya aina mbalimbali.