UN kusaidia Tanzania kufanikisha Ajenda 2030

24 Septemba 2021

Mara baada ya kuhutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76 jijini New York, Marekani, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alikuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
 

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa Alhamisi jijini New York, Marekani imesema katika mkutano huo, Katibu Mkuu Guterres amekaribisha marekebisho makubwa ya kisera yaliyofanyika hivi karibuni katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Marekabisho hayo ni pamoja na usimamizi na udhibiti wa janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.

Halikadhalika walijadili suala la amani na usalama na changamoto zake katika ukanda wa Maziwa Makuu.

Katibu Mkuu Guterres amemhakikishia Rais Samia juu ya usaidizi wa Umoja wa Mataifa kwa Tanzania katika harakati zake za kufanikisha Ajenda 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter