WHO inachunguza hatari za maambukizi ya COVID-19 kwa watoto na barubaru

15 Septemba 2021

Wakati idadi ya wagonjwa wa corona au COVID-19 waliothibitishwa au kukutwa na virusi miongoni mwa watoto imefikiwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu kuzuka kwa janga hilo na tangu kuanza kwa muhula mpya wa masomo katika nchi mbalimbali, shirika la afya duniani WHO linaamini kuwa aina mpya ya virusi vya Corona inaonekana kuwagusa zaidi vbarubaru. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na WHO "Takwimu za kimataifa za matukio ya COVID-19  miongoni mwa vijana barubaru zinaonyesha kwamba watoto wengi wanapima virusi vya COVID-19 , hata hivyo shirika hilo limesema "Utafiti zaidi unahitajika kupata taarifa zaidi.” 

 Mchango wa watoto na barubaru katika maambukizi kwenye jamii 

Licha ya hayo, WHO inasema watoto wa kila rika wanaweza kuambukizwa na wanaweza kusambaza virusi kwa watu wengine.  

Kwa kuongezea, shirika hilo linasema kuna hitaji la haraka la taarifa za kitabibu  kuhusu sababu zinazochangia uwezekano mkubwa wa watoto na vijana barubariu kuambukizwa zaidi virunsi vipya vya  SARS-CoV-2. 

WHO inasema kwa ujumla, maambukizo kwa watoto na barubaru husababisha watu kuugua lakini si mahututi na vifo ni vichache ikilinganishwa na watu wazima.  

Ingawa kutokuwa mahuttuti kwa Watoto na vijana barubaru ni dalili njema  kuna wasiwasi kwamba dalili nyepesi zinaweza kusababisha watoto na vijana wachache kupata vipimo. 

Na hii imesababisha kupungua kwa idadi ya visa vilivyotambuliwa vya maambukizi miongoni mwa watoto na vijana barubaru. 

"Ikiwa watoto na vijana walio na dalili dhaifu au wasio na dalili zote pia huambukiza ugonjwa huo, wanaweza pia kuchangia maambukizi katika jamii," limesema shirika la WHO. 

Sudan Kusini imesalia kuwa moja ya nchi masikini duniani
UNMISS
Sudan Kusini imesalia kuwa moja ya nchi masikini duniani

 Je vipi kuhusu maambukizi kati ya watoto na barubaru? 

Kuhusiana na kusambaa kwa maambukizo miongoni mwa watoto na vijana barubaru, WHO inakumbusha kuwa janga laCIVID-19 limebainika katika shule za upili, kambi za wanafunzi za majira ya joto na vituo vya kulelea watoto, haswa wakati hatua za kujitenga, na kuvaa barakoa havikutumika ili kupunguza hatari. 

Kulingana na shirika hilo la Umoja wa Mataifa, kuna "ushahidi wa awali" unaonyesha kuwa watoto sio waambukizaji wakubwa kama walivyo barubaru na watu wazima.  

Kwa ujumla, watoto na vijana barubaru ambao wameambukizwa virusi vya SARS-CoV-2 wanaweza kuondoa virusi kwa njia zao za hewa na wanaweza pia kuvitoa kwenye kinyesi chao. 

Mwishowe, uhusiano kati ya rika, mzigo wa virusi na maambukizi kwa dalili zote za v irusi vya SARS-CoV-2 haujafanyiwa utafiti wa kutosha, kwa sababu watu wasio na dalili, au wenye dalili ndogo mara chache wanafanyiwa vipimo. kimfumo. 

"Kwa hivyo, uwezekano wa maambukizi ya SARS-CoV-2 katika umri tofauti bado hauna uhakika, haswa kwa sababu ya ugumu wa kutenganisha ushawishi wa sababu za kibaolojia, ubebaji wa virusi hivyo, virusi vyenyewe na mazingira," linabainisha shirika la WHO. 

 Dalili za COVID-19 kwa watoto na barubaru 

Watoto wadogo wa chini ya umri wa miaka mitano, watoto wakubwa, na vijana barubaru wa umri wa kati ya miaka 10 hadi 19 kawaida huwa na dalili chache na na ambazo si kali za maambukizo kuliko watu wazima zaidi ya miaka 25.  

Makundi haya ya umri yana uwezekano mdogo kuliko watu wazima kuwa na COVID-19 ambayo ni kali. 
Ripoti za mapema zinaonyesha kwamba kuna hatari ya kuugua zaid na kuwa na dalili mbaya zaidi kwa Watoto wa chini ya umri wa mwaka mmoja, ingawa tafiti kadhaa zinaonyesha watoto wachanga wa (siku 28 za kwanza za maisha) kuwa na dalili dhaifu. ikilinganishwa na wagonjwa wengine Watoto wa umri wa zaidi yam waka mmoja. 

Hata hivyo WHO inasema "Maambukizi kama ya Delta, yanahitaji uchunguzi zaidi kubaini ikiwa hii itabaki kuwa ndio hali. 

Njia moja ambayo WHO inakumbusha ni kuwa hatari ya kuambukizwa COVID-19 miongoni mwa watoto na batrubaru inategemea hali na kiwango cha maambukizi katika jamii na hatua zinazotekelezwa kudhibiti virusi, lakini pia sababu za mapokezi kwa mtoto na sababu za kibaolojia zinazohusiana na virusi yenyewe.

Lakini, watoto na vijana wa miaka yote wanaweza kuambukizwa na pia kuambukiza SARS-CoV-2 kwa watu wengine. 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter