UNICEF Ghana yarahisisha vijana kupata huduma za afya ya uzazi na masuala ya kujamiiana
Huduma za afya ya uzazi na masuala ya kujamiiana mara nyingi hupata vikwazo hasa pale zinapolenga vijana na barubaru. Hii ni kwa kuzingatia kuwa penginepo pahala ambapo huduma hizo zinatolewa si rafiki kwa vijana na hivyo kuhofia kufuata huduma hizo kunaweza kuwa chanzo kwa wao kubainika jambo ambalo wanadhani si jema kwao.