Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Phumzile Mlambo-Ngcuka:Bado idadi ya wanawake katika uongozi haitoshi

Phumzile Mlambo-Ngucka, Mkurugenzi Mtendaji wa  UN Women akizungumza na wanahabari kuhusu ripoti ya Usawa wa jinsia katika utekelezaji ajenda 2030
UN/Eskinder Debebe
Phumzile Mlambo-Ngucka, Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women akizungumza na wanahabari kuhusu ripoti ya Usawa wa jinsia katika utekelezaji ajenda 2030

Phumzile Mlambo-Ngcuka:Bado idadi ya wanawake katika uongozi haitoshi

Wanawake

Mkurugenzi mtendani wa shirika la Umoja wa Mastaifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women amesema uwakilishi wa wanawake katika uongozi bado hautoshi kote duniani na sasa ni wakati wa kukamilisha malengo ya mkutano wa Beijing kuhusu haki za wanawake katika kila nyanja.

Kupitia ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya wanawake hii leo Bi. Phumzile Mlambo Ngcuka amesema maadhimisho yam waka huu yamekuja wakati ambao ni mgumu kwa dunia na kwa usawa wa kijinsia , lakini katika wakati muafaka wa kupigania hatua za mabadiliko na kuwaenzi wanawake na vijana kwa jitihada zao za kusongesha mbele usawa wa kijinsia na haki za binadamu.

Ameongeza kuwa “Tunachojikita nacho kwa sasa ni uongozi wa wanawake na kuongeza uwakilishi wao katika nyanja zote ambako maamuzi yanafanywa wakati hu una wanaume katika masuala yanayowaathiri wanawake na Maisha yao. Janga la kukosa uwakilishi wa wanawake duniani kote limeendelea kwa muda mrefu sana”

Athari za COVID-19 kwa wanawake 

Tunaposhughulikia athari zilizosababishwa na janga la COVID-19 kwa mamilioni ya wanawake na wasichana na jamii zao, tunatazamia pia fursa nzuri za kizazi cha  usawa na Muungano wa kuchukua hatua kuleta mabadiliko.

“Wakati wa janga hilo, tumeshuhudia kuongezeka kwa unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana na kupoteza elimu kwa wasichana kuongezeka kwa viwango vya kuacha shule, kuongezeka kwa majukumu ya kutoa huduma majumbani na ndoa za utotoni zinaongezeka.” 

Pia amesema dunia inashuhudia makumi ya mamilioni ya wanawake wakitumbukia katika umasikini uliokithiri, kwani wanapoteza kazi zao kwa kiwango kikubwa kuliko wanaume, na wanalipa gharama kwa kukosa fursa na  ujuzi wa kidijitali. 

Shida hizi na zingine nyingi haziwezi kuachwa kwa wanaume peke yao kuzisuluhisha. Amesema Bi. Phumzile na kuongeza kwamba hata hivyo wakati kuna tofauti za kipekee, katika nchi nyingi hakuna idadi kubwa muhimu ya wanawake katika nafasi za kufanya maamuzi na nafasi za uongozi ili kuhakikisha kuwa masuala haya yanawasilishwa na kushughulikiwa vyema na hii imeathiri kasi ya mabadiliko kwa wanawake kwa jumla.

Wanawake wakiwa wamekaa juu ya magunia ya mchele na mahindi huko Wajir, Kenya
FAO/Ami Vitale
Wanawake wakiwa wamekaa juu ya magunia ya mchele na mahindi huko Wajir, Kenya

Pamoja na changamoto kuna cha kujivunia

Mkuu huyo wa UN women ameongeza kusema pamoja na changamoto zote hizo kuna mafanikio ya kusherehekea, ambapo wanawake wamechukua uongozi wa mashirika kama vile Shirika la biashara ulimwenguni WTO, Shirika la Fedha la Kimataifa  IMF na Benki kuu ya Ulaya na tunatarajia uteuzi zaidi kama huu ambao unasaidia kubadilisha picha ya jinsi kiongozi anavyoonekana . 

Walakini hii sio kawaida. Mwaka 2020, kama wastani duniani, wanawake walikuwa asilimia 4.4 ya wenyeviti watendaji au CEO, wakishikilia asilimia 16.9 tu ya viti vya bodi, wakiwa asilimia 25 tu ya wabunge wote wa kitaifa, na asilimia 13 tu ya wasimamizi  au wasuluhishi wa mazungumzo ya amani. 

Na hadi sasa ni nchi 22 tu zina mwanamke kama mkuu wa nchi au Serikali na  katika nchi 119 hawajawahi kupata fursa hiyo jambo ambalo lina athari kubwa kwa matakwa ya wasichana wanaokua. 

Katika mwenendo wa sasa, amdesema Bi. Phumzile hatutaona usawa wa kijinsia katika ofisi za jnyadhifa za juu kabla ya 2150.

UN Women mwaka 2020 mwezi Februari, walitembelea kituo cha Polisi kinachoundwa na wanawake pekee.
UN Women/Ploy Phutpheng
UN Women mwaka 2020 mwezi Februari, walitembelea kituo cha Polisi kinachoundwa na wanawake pekee.

Mwa mukhtada huo amesema “Hali hii inaweza na lazima ibadilike. Kinachohitajika ni utashi wa kisiasa kusaidia kikamilifu na kwa makusudi uwakilishi wa wanawake. Viongozi wanaweza kuweka na kufikia malengo ya usawa, pamoja na kupitia uteuzi wa nafasi zote za watendaji katika ngazi zote za serikali, kama ilivyotokea katika nchi chache zilizo na mmabaraza ya mawazitri yanye usawa wa kijinsia. Hatua maalum zinaweza kufanya kazi, ambapo nchi zimeweka na kutekelezaviti maalum, wamepiga hatua ya maendeleo ya kweli ya uongozi wa wanawake, kama vile wale ambao wana sera za kushughulikia uwakilishi. Ambapo hatua hizi hazipo, maendeleo ni polepole au hata hayapo na hubadilishwa kwa urahisi.”

Amesisitiza kwamba hakuna nchi inayofanikiwa bila ushiriki wa wanawake. “Tunahitaji uwakilishi wa wanawake ambao unaonyesha wanawake na wasichana wote katika utofauti na uwezo wao wote, na katika hali zote za kitamaduni, kijamii, kiuchumi na kisiasa. Hii ndiyo njia pekee ambayo tutapata mabadiliko ya kijamii ambayo yanawajumuisha wanawake katika usawa wa kufanya maamuzi na hutunufaisha sisi sote.”

Wanawake nchini Colombia wakipamba  mji wa Monterredondo kwa ujumbe wa amani.
UN Verification Mission in Colombia/Daniel Sandoval
Wanawake nchini Colombia wakipamba mji wa Monterredondo kwa ujumbe wa amani.

Amehitimisha ujumbe wake kwa kusema kwamba “Haya ndio maono ya zjenda ya 2030 na Malengo ya maendeleo endelevu na maono ya azimio la Beijing na jukwaa la utekelezaji. Ni maono ya asasi za kiraia na umati wa vijana ambao tayari wanaongoza na wa wale wote watakaojiunga nasi katika muungano wa utekelezaji wa kizazi hiki. Tunahitaji hatua madhubuti za maamuzi kote duniani ili kuleta wanawake katika kitovu cha nafasi za kufanya uamuzi kwa idadi kubwa na kama washirika kamili, ili tuweze kupata maendeleo ya haraka kwenye ulimwengu unaojali mazingira, usawa na jumuishi.