Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN iwe mfano kutekeleza usawa wa jinsia- Guterres

Katibu Mkuu wa UN António Guterres (wa 2 kutoka kulia mstari wa mbele) akiwa na wanawake viongozi walio kwenye jopo la viongozi waandamizi kabisa wa UN, hatua ambayo inadhihirisha kauli yake ya kutekeleza usawa wa jinsia kwa vitendo.
UN /Mark Garten

Wanawake

Wahenga walinena kuwa toa kwanza boriti kwenye jicho lako na ndio utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako na ndilo jambo ambalo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameamua kufanya katika kupigia chepuo usawa wa kijinsia!

Umoja wa Mataifa unapaswa kuwa mfano duniani katika kufanikisha usawa wa kijinsia, amesema Katibu Mkuu Antonio Guterres kwenye ujumbe wake wa siku ya wanawake ulimwenguni hii leo. 

Guterres kwenye ujumbe wake anasema ni dhahiri shahiri kuwa mfumo dume umetamalaki kuanzia serikalini, mashirika ya kiraia na yale ya kimatiafa ikiwemo Umoja wa Mataifa na kwamba, “Hoja ya msingi kuhusu usawa wa jinsia ni hoja kuhusu madaraka!”

Sasa anasema basi, ameanza kuchukua hatua ili utekelezaji wa uwiano wa 50 kwa 50 kwenye uongozi uanzie pale anapoongoza yeye, Umoja wa Mataifa kwani , “Tayari tumefikia idadi sawa ya viongozi waandamizi wa la juu kabisa wa UN. Punde tutafikia uwiano huo kwenye ngazi ya viongozi wa UN katika nchi wanachama. Lengo ni kuwa na usawa huo kwenye ngazi zote za Umoja wa Mataifa.”  Amesema Katibu Mkuu.

Wanawake Brazil waandamana kupigania haki za wanawake
UN Women/Bruno Spada
Wanawake Brazil waandamana kupigania haki za wanawake

Guterres anaamini wanawake wakipatiwa uongozi ni rahisi kukabili vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kingono vitendo ambavyo amesema hatovumilia kabisa.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen, Phumzile Mlambo-Ngucka ametumia fursa ya kupiga kengele kwenye soka la fedha la Nasdaq jijini New York, Marekani kueleza furaha yake kwa kuwepo kwenye soko hilo la fedha.

Amesema kuwa, UN Women inafurahia kushirikiana na Nasdaq na kuadhimisha sherehe hizi leo. Kwa sababu ni fursa ya kutathmini wanawake walikotoka. Napongeza pia kwa kazi yenu na ushiriki wa wanawake siyo tu kusongesha bishara nzuri bali pia kuweka mazingira kwa wanawake kupata fursa maeneo yenye pesa.”

Mcheza filamu na mwanaharakati Danai Gurira (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women Phumzile Mlambo-Ngucka, (katikati), pamoja na mcheza filamu na mwanaharakati Reese Witherspoon (kulia) wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hii leo UN.
UN Women Twitter