Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maskini wataongezeka kufikia zaidi ya watu bilioni moja. Nchi maskini kuathirika zaidi-UN  

Wavulana wawili katika kambi ya Loda ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
UNICEF/Desjardins
Wavulana wawili katika kambi ya Loda ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maskini wataongezeka kufikia zaidi ya watu bilioni moja. Nchi maskini kuathirika zaidi-UN  

Ukuaji wa Kiuchumi

Ripoti mbili kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa zilizotolewa hii leo, kwa namna tofauti zimeonesha namna athari za ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona, zikavyosababisha kuporomoka kwa nguvu ya uchumi ya watu wengi na hivyo kuwaingiza katika umaskini uliokithiri. 

Utafiti mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP umesema, “watu zaidi ya milioni 207 wanaweza kusukumwa katika umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030, kwa sababu ya athari mbaya ya muda mrefu ya janga la virusi vya corona, na hivyo kufanya jumla ya zaidi ya watu bilioni moja maskini.”  

Kwa mujibu wa utafiti huo, hali kama hiyo "ya uharibifu mkubwa" inaweza kumaanisha kuchelewa kuishinda COVID-19, ikitarajiwa kuwa asilimia 80 ya janga la uchumi inayosababishwa na janga itaendelea zaidi ya muongo mmoja. 

Wazazi wa Rani wanaishi chini ya kiwango cha umasikini na wanategemea programu ya mlo wa mchana ya WFP.
WFP/Isheeta Sumra
Wazazi wa Rani wanaishi chini ya kiwango cha umasikini na wanategemea programu ya mlo wa mchana ya WFP.

SDGs ni tumaini 

Hata hivyo UNDP inasema kuzingatia kwa nguvu kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, kunaweza kupunguza kasi ya umaskini uliokithiri , kuwaondoa watu milioni 146 kutoka kwa mtego huo wa umaskini na hata kuzidi mwelekeo wa maendeleo ambayo ulimwengu ulikuwa kabla ya janga hilo la COVID-19.  

Mkuu wa UNDP Achim Steiner ameangazia kuwa janga la COVID-19 ni "kidokezo tu" mstakabali wa siku zijazo utategemea maamuzi yanayotolewa leo.  

"Kama utafiti huu mpya wa umaskini unavyoonesha, janga la COVID-19 ni kidokezo, na machaguo wanayoyafanya viongozi hivi sasa yanaweza kuupeleka ulimwengu katika mwelekeo tofauti. Tunayo nafasi ya kuwekeza katika muongo mmoja wa hatua ambayo sio tu inasaidia watu kupona kutoka kwa COVID-19, lakini hiyo inaweka upya njia ya maendeleo ya watu na sayari kuelekea mustakabali mzuri, wenye mnepo na kijani." Amesema Steiner.  

Utafiti huo unaolenga kutathimini athari za hali tofauti za mapambano dhidi ya COVID-19 na athari nyingi za janga hilo katika miaka kumi ijayo, umeaandaliwa kwa pamoja kati ya UNDP na Kituo cha Pardee cha Mstakabali wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Denver Marekani.  

Utafiti wa UNCTAD 

Zaidi ya watu maskini milioni 32 wanakabiliwa na kurudishwa katika umaskini uliokithiri kwa sababu ya COVID-19, wanauchumi wakuu wa Umoja wa Mataifa wakionesha data inayoonyesha kuwa janga hilo linaweza kusababisha mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi kwa miongo kadhaa miongoni mwa nchi zilizoendelea au zenye uchumi mdogo. 

Katika wito wa uwekezaji wa haraka na msaada kutoka kwa jamii pana ya kimataifa, shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD limeonya kuwa cvirusi vya corona vimehatarisha kurejesha nyuma hatua kubwa iliyokuwa imefikiwa, kwenye upunguzaji umaskini, lishe na elimu.  

 “Janga la COVID linazipeleka nchi maskini katika  janga lao baya zaidi la kiuchumi  katika miaka 30, na Pato la Taifa, GDP linalotarajiwa kushuka kwa asilimia 2.6 mwaka huu." Amesema Mukhisa Kituyi, Katibu Mkuu wa UNCTAD, wakati wa mkutano wa waandishi wa habari.