Chuja:

LDCs

Mkunga Helen Danies anazungumza na mama  katika wodi ya kinamama hospitalini
UNICEF/UN0159224/Naftalin

Kituo kimoja cha afya kati ya vinne hakina huduma ya maji-UNICEF/WHO.

Kati ya vituo vinne vya afya duniani kote, kimoja kinakosa huduma za maji, hali inayowaathiri zaidi ya watu bilioni mbili. John kibego na taarifa kamili. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya pamoja iliyotolewa usiku wa kuamkia leo mjini Geneva Uswisi na New York Marekani na shirika la afya duniani WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Sauti
3'5"
Picha: IFAD/GMB Akash

Bei ya vyakula imepanda

Kuagiza chakula kutoka nje kunaongeza  mzigo mkubwa kwa mataifa maskini duniani, imesema ripoti mpya kuhusu hali ya chakula iliyotolewa na  shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa la FAO. Mathalani kwa ujumla tangu mwaka 2000 hadi mwaka jana, mataifa duniani yalitumia dola trilioni 1.43 kuagiza chakula nje ya nchi, kiwango ambacho ni ongezeko mara tatu huku gharama ikiwa imepanda mara tano zaidi kwa mataifa ambayo  yanakabiliwa na zaidi na uhaba wa chakula.

 

Sauti
2'9"
UN/Eskinder Debebe

Nchi zaidi zapendekezwa kuondolewa orodha ya LDCs

Hii leo kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu sera za maendeleo, CDP inatangaza nchi ambazo zimependekezwa kuondolewa kutoka katika kundi la nchi zilizo katika harakati za kujikwamua kiuchumi, LDCs.

Nchi hizo 4 ambazo ni Bhutan, Kiribati, São Tomé na Principe pamoja na visiwa vya Solomon, zimetangazwa baada ya kukidhi vigezo viwili kati ya vitatu ambavyo hutumiwa kubaini iwapo nchi bado ni LDCs au la.

Vigezo hivyo ni pamoja na pato la ndani la taifa, hali ya elimu na afya kwa wananchi wake pamoja na uchumi stahimilivu.

Sauti
2'41"