Skip to main content

Chuja:

MUKHISA KITUYI

Vijana wa Afrika wapelekwa kampasi ya Ali Baba kujifunza biashara za kielektroniki

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imezungumzia ushirikiano wake na kampuni ya Ali baba katika kuinua uwezo wa vijana wa Afrika kwenye kutumia majukwaa ya kieletroniki kuuza bidhaa zao.

Katibu Mkuu wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi amezungumzia mradi huo akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Amesema wamanzisha mradi huo na Jack Ma, kiongozi wa kampuni ya Ali Baba ambapo vijana kutoka Afrika wanakwenda jimboni Hangzhou kujifunza jinsi ya kujenga majukwaa ya biashara mtandaoni.

Sauti
1'1"
Picha ya UM

Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja umeshuka kote duniani 2017

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya  kamati ya maendeleo na biashara ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi.

Ripoti hiyo“Uwekezaji na sera mpya za viwanda “, imetathimini hali ya uwekezaji duniani katika  kipindi cha kati ya  2016 na 2017. Katibu Mkuu wa UNCTAD, Mukhisa Kituyi, amesemaushukaji wa FDI na pia kudorora kwa makampuni tanzu duniani vinaleta wasiwasi hususan katika nchi zinazochipukia kiuchumi

Sauti
2'31"