Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 imeangusha kwa asilimia 49 aina zote za uwekezaji wa nje wa nchi zilizoendelea.

Uwekezaji mkubwa kama huu wa bwawa katika Mto Nura nchini Kazakhstan mara nyingi unahitaji uwekezaji wa moja kwa moja wa nje.
World Bank/Shynar Jetpissova
Uwekezaji mkubwa kama huu wa bwawa katika Mto Nura nchini Kazakhstan mara nyingi unahitaji uwekezaji wa moja kwa moja wa nje.

COVID-19 imeangusha kwa asilimia 49 aina zote za uwekezaji wa nje wa nchi zilizoendelea.

Ukuaji wa Kiuchumi

Mtiririko wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni kimataifa, FDI, umepungua kwa asilimia 49 katika nusu ya kwanza ya 2020 ikilinganishwa na mwaka 2019, kwa sababu ya kuanguka kwa uchumi kutokana na COVID-19, umebaini utafiti wa hivi karibuni wa  Monitor mwelekeo wa uwekezaji uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD na kutolewa leo tarehe 27 Oktoba 2020. 

Kufuatia janga hilo la virusi vya corona, kufungwa kwa mipaka kote duniani, kumezorotesha miradi iliyopo ya uwekezaji na matarajio ya mtikisiko mkubwa wa uchumi ulisababisha biashara za kimataifa kutathimini miradi mpya. 

James Zhan, Mkurugenzi wa uwekezaji na biashara wa UNCTAD, anasema, "kupungua kwa uwekezaji wa moja kwa moja wa kimataifa ni mkubwa zaidi kuliko tulivyotarajia, hasa katika uchumi ulioendelea. Mataifa yaliyoendelea yalikabili dhoruba vizuri zaidi kwa nusu ya kwanza ya mwaka. Matazamio bado yanabaki bila uhakika." 

Hata hivyo ripoti imeonesha kuwa nchi za uchumi ulioendelea zilishuhudia anguko kubwa la uwekezaji wan je kufikia kiasi kinachokadiriwa kuwa dola bilioni 98 za kimarekani katika kpindi cha miezi 6, ambalo ni anguko la asilimia 75 ikilinganishwa na mwaka 2019.  

Mwelekeo huo uligongelewa zaidi na msumari wa mapato mabaya sana katika uchumi wa Ulaya, hasa Uholanzi na Uswisi. Mtiririko wa uwekezaji wa nje kwenda Amerika Kaskazini ulipungua kwa asilimia 56 hadi dola za kimarekani bilioni 68. 

Wakati huo huo, kupungua kwa asilia 16 kwa mtiririko wa uwekezaji wa moja kwa moja wan je kwa uchumi unaoendelea kulikuwa chini ya ilivyotarajiwa, kwa sababu ya uwekezaji thabiti nchini China. Mtiririko ulipungua kwa asilimia 12 tu katika Asia lakini ilikuwa asilimia 28 chini kuliko katika mwaka 2019 barani Afrika na asilimia 25 chini katika Amerika ya Kusini na Karibea. 

Matazamio ya kipindi kilichosalia cha mwaka, bado yanabaki kuwa hasi, imeeleza UNCTAD.