Uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje umerejea katika hali ya kabla ya COVID-19: UNCTAD
Mpangilio wa uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje FDI umejikwamua na kurejea katika hali ya kabla ya janga la COVID-19 mwaka jana na kufikia kiwango cha dola trilioni 1.6 lakini matarajio kwa mwaka huu ni mabaya kwa mujibu wa ripoti mpya ya uwekezaji duniani iliyotolewa leo na kamati ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo ya uchumi na biashara UNCTAD.