Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka uimbaji jukwaani hadi kuuza vijiko mitaani, kulikoni? COVID-19

Gerald Mutabaazi akionesha miiko ambayo ametengeneza baada ya kugeukia kazi ya useremala kufuatia COVID-19 kuvuruga kazi yake ya uanamuziki.
UN/ John Kibego
Gerald Mutabaazi akionesha miiko ambayo ametengeneza baada ya kugeukia kazi ya useremala kufuatia COVID-19 kuvuruga kazi yake ya uanamuziki.

Kutoka uimbaji jukwaani hadi kuuza vijiko mitaani, kulikoni? COVID-19

Ukuaji wa Kiuchumi

Nchini Uganda, baada ya janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 kukwamisha harakati za vijana ikiwemo wanamuziki kuendesha shughuli zao, kijana mmoja mwanamuziki ameamua kurejea katika kazi yake ya useremali ili aweze kutunza familia yake. 

Mwanamuziki huyo Gerald Mutabaazi al maarufu Katobantobe hakukubali COVID-19 kumuumbua. 

Mlipuko wa Corona mwezi Machi mwaka huu, ulimlazimu kurejea kijijini Buchunga. Sasa kazi yake ni kutengeneza vifaa vya jikoni kutokana na mbao na vijiti ambavyo yeye mwenyewe hutafuta msituni na kisha kutembeza bidhaa hizo mjini Hoima, 

Bwana Mutabaazi anasema kuwa,  “kwa uhakika mlipuko wa corona ulipotangazwa, mimi kama msanii hapa niliona kwamba sipaswi kukaa chini kuela mikono kwa sababu walifunga klab za muziki, wakafunga hafla zote na hatukuwa na njia yoyote ya kipato. Nilisema hapana kipaji hua ni kipaji na Mungu akikufungulia hua amekufungulia nafasi nikaamua kuanza sanaa hii ya kufundi seremala. Tuliungana na mwenzagu chini ya timu yetu ya One Hundred Flowers” 

Vijiko vya kupakulia chakula na vile vya kukorogea mchuzi ni miongoni mwa bidhaa zake sokoni. Katobantobe anajali familia yake kinyume na matarajio ya wengi waliokuwa wanafuatilia familia yake akisema kuwa, “sasa nina mke na watoto na ni lazima nitafute mahitaji ya familia. Ndio maana baadhi ya waimbaji wanapitia kipindi kigumu kwa sababu walitegemea kazi hiyo tu bia kupanga vinginevyo kubuni kazi. Nawatolea wito huko nafuteni kazi ya mikono kama mbadala, uimbaji ni kipaji kipo hakiozi” 

Kuhusu kusongesha vipaji hivi viwili tofauti baada ya Corona, anasema, “kwa ukweli nitaendelea na uimbaji na pia nafikiria kuanza uchezaji wa filamu. Useremala pia utaendelezwa sana kwa sababu hiyo ni biashara mabayo imeanza mara moja ikiwa na baraka za Yesu”