UN wawapongeza vijana wa jamii ya asili kwa kutokubali ukandamizaji wa jamii zao
Hii leo ni siku ya jamii ya watu wa asili duniani ambapo maudhui ni vijana, ikisherehekea vijana wa jamii ya asili na dhima yao katika kuleta mabadiliko na kuumba mustakabali wa dunia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa ujumbe wake.
Katika ujumbe wake wa siku hii iadhimishwayo tarehe 9 mwezi Agosti ya kila mwaka, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anasema duniani kote watu wa jamii ya asili wanakabiliwa na changamoto, ardhi na rasilimali zao zikitishiwa haki zao zikikandamizwa na changamoto yao ya kila uchao ya kuenguliwa na kutengwa.