Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 bado ipo na athari zake zitakuwa za miongo:WHO 

Muhudumu wa afya akipima joto la mwili la mgonjwa katika hospitali kwenye jimbo la Nonthaburi Thailand
UN Women/Pathumporn Thongking
Muhudumu wa afya akipima joto la mwili la mgonjwa katika hospitali kwenye jimbo la Nonthaburi Thailand

COVID-19 bado ipo na athari zake zitakuwa za miongo:WHO 

Afya

Kamati ya dharura ya shirika la afya duniani WHO ya kupambana na janga la corona au COVID-19 imekutana mjini Geneva Uswis katika kikao maalum kilichoitishwa na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

 

 

 

Ikishukuru juhudi kubwa zinazofanywa na shirika hilo katika vita dhidi ya COVID-19, kamati hiyo imeweka bayana kwamba bado hakujafikiwa mwisho wa kushuhudia mgogoro huu wa afya ya umma ambao hadi kufikia sasa umeshakatili watu zaidi ya milioni 17 na kukatili maisha ya watu zaidi ya 650,00.

Kamati hiyo imekutana chini ya kanuni za kimataifa za afya (IHR) 31 Julai na huu ni mkutano wao wa nne. 

Juhudi endelevu zahitajika 

Katika taarifa yao iliyochapishwa leo Jumamosi kufuatia mkutano wao kamati hiyo imegusia “Matarajio ya muda ambao janga hilo 

litaendelea na kutaja umuhimu wa kuwa na juhudi endelevu za kijamii, kitaifa, kikanda n kimataifa.” 

Baada ya madala mrefu na kutathimini ushahidi kamati hiyo kwa pamoja bila kupingwa imeafiki kwamba mlipuko bado unaendelea kuwa 

dharura ya kiafya yenye kutia hofu ya kimataifa (PHEIC) na Dkt. Tedros amekubali ushauri huo. 

Mkuu wa WHO alitangaza janga lacorona kuwa dharura ya kimataifa yenye kuta hofu tarehe 30 Januari mwaka huu wakati ambao 

kulikuwa na wagonjwa kidogo chini ya 100 na hakukuwa na vifo vyovyote nje ya China. 

COVID-19 ni janga la karne 

“Janga hili ni moja ya majanga ya karne ya mgogoro wa kiafya ambalo athari zake zitadumu kwa miongo” Dkt. Tedross ameiambia 

kamati hiyo ktika taarufa yake. Ameongeza kuwa “Nchi nyingi ambazo ziliamini kuwa zimelivuka janga hili sasa wanahaha na mlipuko 

mpya. Baadhi ya nchi ambazo hazikuathirika sana mwanzoni sasa wanashuhudi idadi ikiongezeka ya wagonjwa na vifo. Na baadhi ya nchi zilizokuwa na milipuko mikubwa sasa zinafanikiwa kupunguza idadi ya wagonjwa na vifo.” 

Mapendekezo 

Kamati hiyo imetoa mapendekezo mbalimbali kwa WHO na nchi wanachama. Imelishauri shirika hilo la afya kendelea kuchagiza mashirika ya kikanda na kimataifa na washirika wengine kwa ajili ya maandalizi na hatua za kupambana na gonjwa hilo lakini pia kuendelea kuwasaidia

nchi wanachama katika kuhakikisha huduma za afya, huku pia wakiendelea na shughuli za utafiti na hatimaye kufikia vipimo, matibabu na chanjo.