Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakielimishwa na kujumuishwa Vijana ni chachu kubwa katika SDGs:YUNA

Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs
UN SDGs
Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs

Wakielimishwa na kujumuishwa Vijana ni chachu kubwa katika SDGs:YUNA

Ukuaji wa Kiuchumi

Vijana wanaweza kuwa chachu kubwa katika utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s  mwaka 2030 endapo wataelimishwa kujumuishwa na kupewa fursa. 

Kauli hiyo imetolewa na Jolson Masaki, mwenyekiti wa asasi ya Umoja wa Mataifa ya vijana (YUNA) nchini Tanzania ambaye ni miongoni mwa washiriki wa jukwaa la vijana la baraza la kiuchumi na kijamii la umoja wa Mataifa ECOSOC, 2019.

Akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili kandoni mwa jukwaa hilo linalokunja jamvi hii leo mjini New York Marekani baada ya kumulika vijana na SDGs, Jolson amesema kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu inapaswa kupewa uzito si tu kwa ajili ya vijana bali pia mustakabali wa jamii zao