Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wawekeni wanawake na wasichana katika kitovu cha mapambano dhidi ya COVID-19: Katibu Mkuu wa UN

Mama na bintiye wakiwa wamevaa barakoa kujilinda dhidi ya virusi vya corona katika kituo cha afya Abidjan, Côte d'Ivoire.
© UNICEF/Frank Dejongh
Mama na bintiye wakiwa wamevaa barakoa kujilinda dhidi ya virusi vya corona katika kituo cha afya Abidjan, Côte d'Ivoire.

Wawekeni wanawake na wasichana katika kitovu cha mapambano dhidi ya COVID-19: Katibu Mkuu wa UN

Wanawake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo Alhamis ameonya kuwa hatua zilizopigwa katika usawa wa kijinsia na haki za wanawake vilivyofikiwa kwa miongo kadhaa, viko hatarini kurejea nyuma kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, COVID-19.

Onyo hilo kali la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa liko katika muhtasari wa sera ambayo inaelezea jinsi ugonjwa mpya unavyoongeza zaidi pengo la usawa ambalo limekuwepo tangu na inaongeza athari zake kwa maisha ya wanawake na wasichana. 

“Ninazisihi serikali kuwaweka wanawake na wasichana katika kitovu cha juhudi za kupona kutokana na coronavirus">COVID-19. Hilo linaanza na wanawake na viongozi, walio na uwakilishi sawa na nguvu ya maamuzi.” Bwana Guterrres amesema kwa njia ya video kusindikiza uzinduzi wa ripoti.

Madhara ya COVID-19 

Mlipuko huu unatokea katika mwaka ambao dunia inaadhimisha miaka 25 ya Mkutano wa wanawake uliofanyika Beijing kwa ajili ya hatua kuelekea haki za wanawake na usawa wa kijinsia.

COVID-19 imeripotiwa katika kila pembe ya dunia na takribani wagonjwa milioni 1.5 na zaidi ya vifo 85,000 vimetrokea tangu uginjwa huo ulipoibuka mwezi Desemba mwaka jana 2019 nchini China.

Wakati kila mtu ameathirika kwa namna moja au nyingine, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza zaidi kuhusu madhara makubwa ya ugonjwa huo kwa wanawake na wasichana kote duniani kuanzia ktika upande wa afya na uchumi, usalama na ulinzi wa kijamii.

“Takribani asilimia 60 ya wanawake kote duniani wanafanya kazi katika uchumi usio rasmi, wakipata kipato kidogo, akib kidogo na wakiwa katika hatari ya kuangukia katika lindi la umaskini. Wakati masoko yakianguka na biashara zikifunga, mamilioni y kazi za wanawake zimetoweka. Wakati huo huo wakati wanawake wanapoteza kazi zao za malipo, kazi za wnawake za kutokulipwa zimeongezeka kwa kasi kutokana na shule kufungwa n ongezeko la mahitaji ya watu wa umri mkubwa.” Amesema Bwana Guterres.

Kwa hivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka seikali zote kuwaweka wanawake katika uongozi na kuwatumia katika maamuzi. 

“Kwa hivyo basi tunapaswa kuhakikisha wanawake wanajumuishwa katika maamuzi yote. Hii ndiyo njia pekee ya kurejea upya katika ubora kwa wote.” Amesisitiza.